Home BUSINESS WAFANYA BIASHARA WAKUMBUSHWA KUHUSU DHANA YA WAMILIKI MANUFAA

WAFANYA BIASHARA WAKUMBUSHWA KUHUSU DHANA YA WAMILIKI MANUFAA

Katika jitihada za kuendeleza sekta ya biashara nchini, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imeendesha semina maalum kwa wadau wa biashara katika kuwaelimishaji juu ya dhana ya Wamiliki Manufaa iliyofanyika leo tarehe 20 Februari, 2024 katika ukumbi wa Royal Tughimbe Hotel jijini Mbeya.

Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara Bw.Isdori Nkindi amesema, mwaka huu BRELA imejikita katika kuangazia changamoto zinazojitokeza wakati wa kufanya Usajili ili kuona namna gani wanaweza kuepukana na vitendo hatarishi hii ni kutokana na baadhi ya kampuni nchini kutumika vibaya kwa kufanya vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu, kufadhili vitendo vya ugaidi na ukwepaji wa kodi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa semina hiyo, washiriki wa mafunzo hayo wameiipongeza BRELA kwa kuandaa semina hiyo iliyowaleta pamoja wadau wa sekta ya biashara Jijini Mbeya kujadili namna ya kuongeza mchango katika maendeleo ya biashara hususani katika kukuza uchumi nchini.

Mmoja wa wafanya biashara hao, Bw. Tumaini Yolim alisema kuwa ni muhimu kuwepo kwa mashirikiano ya karibu kati ya BRELA na wafanyabiashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi utakao wezesha kutatua changamoto za wafanyabiashara kwa wakati.

Aidha Mmiliki wa Kampuni ya Mghaka, Bw. Peter Wegesa Chacha amesema kuwa BRELA iwe mstari wa mbeke katika kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kuweza kusajili biashara zao kwakuwa baadhi yao wamekuwa waoga kurasimisha biashara zao hii ni kutokana na uelewa mdogo wa kujua umuhimu huo

Mbali na utoaji mafunzo, BRELA itatoa huduma za papo kwa papo kwa wafanyabiashara kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2024 katika viwanja vya Kabwe jijini Mbeya.

Previous articleMKATABA BAINA YA NHIF NA APHFAT HAUJAVUNJWA – Dkt. SAGWARE
Next articleRAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MH DKT. MWINYI APOKEA WAGENI MBALIMBALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here