Home BUSINESS WABUNGE WA AFRIKA MASHABIKI WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI BANDARI YA DSM

WABUNGE WA AFRIKA MASHABIKI WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI BANDARI YA DSM

Na: Mwandishi wetu.

kamati ndogo ya mawasiliano, Biashara na uwekezaji ya Bunge la Afrika Mashariki imefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kulidhishwa na utendaji kazi wa bandari hiyo huku wakiahidi ushirikiano zaidi katika kuendelea kuboresha ushirikiano katika biashara.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo februari 8,2024 Mwenyekiti wa kamati hiyo Rutazana Francine amesema ziara imekuja baada ya kukutana na kuzungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na waendeshaji lengo likiwa kujua wanafaidikiaje na utendaji kazi wa centre cordial.

“Tumekuja hapa jijini tangu Februari 4 tulikuja kukutana na wafanyabiashara na wanetuambia vitu vingi kuhusiana na utendaji kazi wa bandari ikiwemo kuchelewa kwa mizigo yao tukaona leo tuje hapa kutembelea kiukweli tumeridhishwa na utendaji kazi wao ni mzuri na changamoto chache tulizoziona tutazishughulikia zile za kisera tutaona namna nzuri ya kuzishughulikia kwa haraka”amesema Francine.

Amesema pamoja na changamoto zinazowakabili kama bandari bado wanajitahidi kutoa huduma nzuri na kuwanufaisha nchi zote zinazotumia central cordial ikiwemo nchi za Rwanda,Burundi,kongo,Uganda na Sudani kusini.

Kwa upande wake mwakilishi wa bunge la EALA kutoka Kenya David ole Sankoo amepongeza utendajikazi wa bandari huku akitoa rai kwa serikali kuzidi kuwekeza kwenye Uchumi wa bluu kwa kutafuta wataalam zaidi kwani hakuna nchi nyingine yenye bahari nyingi kama Tanzania.

Akizungumzia changamoto za kibiashara katika central cordial amesema watatunga sheria zitakazosaidia nchi kufanyakazi pamoja na wafanyabiashara kupata huduma bora.

Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bandari Musa Biboze amesema wamefurahishwa na ziara hiyo kwani itawasaidia kuongeza ufanisi katika bandari hiyo ili waweze kuhudumia nchi nyingi zaidi.

Amesema bandari bandari imeendelea kujipanga kuhudumia meli nyingi zaidi na zenye ukubwa ili kuweza kuhudumia mizigo mingi zaidi na kutolewa kwa wakati.

“Sisi kama Bandari tumejipanga kuweza kutoa huduma bora wa wateja wetu wote wa East Afrika lakini pia tuwaombe kama walivyoziona changamoto ambazo wameahidi kutusaidia ikiwemo ya utungaji wa sheria zitakazosaidia ufanyaji wa biashara kuwa rahisi wazishughulikie kwa wakati ili tuendelee kutoa huduma kwa wananchi wote”Amesema Biboze.

Akizungumzia ucheleweshwaji wa mizigo amesema bandari wameendelea kuboresha ufanisi wa kazi zao ambapo wametoa siku 5 kwa mizigo ya ndani kutolewa huku ya nje inategemea na mikataba yao kwani kuna nchi wanamikataba ya siku 14 huku nyingine ikiwa siku 30.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here