Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Carbonovia ya nchiniĀ Uingereza, inayohusika masuala ya biashara ya hewa ukaa (carbondioxide) Dk. Mike Mason akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona jijini Tanga alipotembelea ofisi za bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya utafiti wa kuzalisha protini kutokana na mabaki ya mkonge, wengine ni watumishi wa TSB na Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST).
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Saddy Kambona akipokea nzi chuma (black soldier flies) na mbolea kutoka kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD), katika Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST), kilichopo mkoani Arusha, Bi. Aziza Konyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyefanya utafiti huo kwa kuongeza thamani kwa kutumia mabaki ya Mkonge (sisal waste).
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Carbonovia ya nchiniĀ Uingereza, inayohusika masuala ya biashara ya hewa ukaa (carbondioxide) Dk. Mike Mason akimwonyesha protini iliyozalishwa na mabaki ya mkonge (sisal waste) Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona jijini Tanga alipotembelea ofisi za bodi hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya utafiti wa kuzalisha protini hiyo ambayo ni gharama nafuu zaidi, wengine ni watumishi wa TSB na Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST).
Hatua hiyo ni tofauti kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD), katika Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) kilichopo mkoani Arusha, Aziza Konyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), amefanya utafiti na kuzalisha nzi chuma (black soldier flies) na mbolea kwa kuongeza thamani kwa kutumia mabaki hayo ya mkonge.
Akizungumza baada ya kikao cha uwasilishaji wa ugunduzi wa utafiti huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amesema utafiti huo ambao umesajiliwa kwa hati miliki pia umebaini licha ya kuzalisha nzi chumaa hao ambao hutumika kama protini kwenye chakula cha mifugo lakini pia mabaki ya chakula wanachokula nzi chuma hao ni mbolea nzuri inayotumika katika mazao mbalimbali.
āBodi imepokea wasilisho la utafiti huo na imefurahi kuona kwamba zao la mkonge linazidi kupata thamani kwa sababu tumezoea baada ya kupatikana singa basi kinachobaki chote ni uchafu kinatupwa.
āTSB ina mahusiano ya muda mrefu na Chuo cha Nelson Mandela katika kufanya tafiti mbalimbali kuhusu uongezaji thamani wa zao la mkonge. Kwa hiyo Aziza chini profesa wake Anthony Mshandete na Revocatus Machunda amefanya utafiti wa kuzalisha nzi chuma (black soldier flies) kutokana na mabaki ya mkonge (sisal waste) ambayo hutumika kama protini kwenye chakula cha mifugo jamii ya ndege wanyama na binadamu,ā amesema Kambona.
Utafiti huu ni wa pili kufanyika na chuo hicho ambapo utafiti wa kwanza unatekelezwa na chuo hicho kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark kupitia Shirika lake la Maendeleo (Danida), ambapo umejikita katika maeneo matatu ambayo ni uzalishaji gesi asilia, ujenzi na kile kitakachozalishwa kutokana na gesi asilia