Home LOCAL UHUSIANO WA TANZANIA NA URUSI KUBORESHWA KUNUFAISHA PANDE ZOTE – NCHIMBI

UHUSIANO WA TANZANIA NA URUSI KUBORESHWA KUNUFAISHA PANDE ZOTE – NCHIMBI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa CCM, chini ya Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kudumisha uhusiano na urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi, ukilenga kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, ambapo amesisitiza kuwa kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kutaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake na kuufanya kuwa wa moja kwa moja zaidi.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Alhamis, Februari 23, 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, pamoja na kurejea kumbukumbu za uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Urusi, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambao mwaka huu unafikisha miaka 62, walizungumzia maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa kazi na Serikali za nchi hizo, chini ya uongozi wa vyama vinavyoongoza nchi hizo, Chama Cha Mapinduzi na United Russia, mtawalia.

Kwa upande wake, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, mbali ya kumpongeza na kumtakia kila la heri Balozi Dk. Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, ameelezea uhusiano wa muda mrefu wa Urusi kwa Tanzania na nchi za Afrika, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambapo ilikuwa mojawapo ya nchi za mwanzo kuitambua Tanganyika huru, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Vladimir Vladimirovich Putin, na mazingira mazuri ya uwekezaji, biashara na uchumi ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Urusi iko tayari kuendelea kuenzi na kuimarisha uhusiano utakaonufaisha pande zote mbili.




Previous articleMAJALIWA ATEMBELEA MAABARA YA KOMPYUTA SHULE YA WASICHANA RUANGWA
Next articleGGML, CHEMBA YA MIGODI WAJIPANGA KUANDAA MITAALA YA WATALAAM UCHIMBAJI CHINI YA ARIDHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here