Dar-es-Salaam,Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo imefanya majaribio ya Treni ya umeme ya SGR kutoka Dar-es-Salaam mpaka Morogoro lengo ni kuanza safari hivi karibuni.
Akizungumza na wanahabari, Leo Februari 26, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema mradi unaendelea vizuri na amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa pamoja nao kwa kipindi chote Cha mradi huo mkubwa unaendeleaje na ujenzi.
“Leo ni siku muhimu sana katika Taifa na uongozi wa awamu ya sita ikiwa Leo ni muendelezo wa majaribio ya treni hii ya umeme (SGR) ambapo tunawaambia Watanzania wote kwa ujumla kuwa reli yao inaelekea katika hatua ya kwanza rasmi kama maagizo ya mheshimiwa Rais alivyoyatoa ya kwamba mpaka mwishoni mwa mwezi wa saba tuwe tumeshaanza kutoka Dar-es-Salaam mpaka Dodoma.
“Lakini katika ujenzi wetu tunajenga kwa vipande Kuna kipande cha kwanza cha kutoka Dar-es-Salaam mpaka Morogoro,lakini kipande kingine cha pili Cha kutoka Morogoro mpaka Makutupora, vipande vingine vinaendelea kutoka Makutupora kwenda Tabora,Isaka, Mwanza na Tabora kwenda Kigoma.
“Na hivi karibuni tutasaini mkataba wa kutoka Uvinza kwenda Msongati kwa maana ya kuunganisha na Burundi baadaye itaenda mpaka DR Congo,”amesema Kadogosa.