Home LOCAL RAIS SAMIA: TANZANIA KUWA MIONGONI YA NCHI 20 ZINAZOKUA KIUCHUMI

RAIS SAMIA: TANZANIA KUWA MIONGONI YA NCHI 20 ZINAZOKUA KIUCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kukabidhiana zawadi katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Malkia Sonja mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme, Norway wakati wa ziara yake ya Kitaifa tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mfalme Harald V wa Norway wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika eneo la Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kwa mwaka 2024 Shirika la Fedha Duniani (IMF) limesema kuwa Tanzania inatarajia kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani.

Rais Samia amesema hiyo ni fursa kwa wawekezaji wa Norway nchini Tanzania kwani pia ina mazingira mazuri ya kisiasa, kijiografia na kiuchumi.

Wakati akihutubia Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika jijini Oslo, Rais Samia amebainisha zipo kampuni kadhaa za Norway zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kisiasa Tanzania ina amani chini ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye kuzingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.

Kwa upande wa kijiografia, Rais Samia amesema Tanzania inafaa kwa uwekezaji kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa manane ya Afrika inayopakana nayo.

Kiuchumi Tanzania ina sera nzuri na imara za kiuchumi na kifedha huku ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) ukirejea kwenye 5.2% kwa mwaka. Unatarajiwa kufikia zaidi ya 6% kwa mwaka ujao kama ilivyokuwa kabla ya COVID 19.

Rais Samia amesisitiza fursa tano za kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati
mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na
usafirishaji.

Rais Samia ameanza ziara ya Kitaifa nchini Norway kwa muda wa siku mbili baada ya kutoka kwenye ziara ya Kihistoria huko Vatican ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleRAIS SAMIA NA MWENYEJI WAKE MFALME HALALD WA (V) WA NORWAY ALIPOWASILI JIJINI OSLO
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA KATIKA JUKWAA LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA NORWAY JIJINI OSLO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here