Home LOCAL NDUGU WAKASUVI ATAKUMBUKWA DAIMA-MAJALIWA

NDUGU WAKASUVI ATAKUMBUKWA DAIMA-MAJALIWA

*_Ni kutokana na mchango wake kwenye kusimamia sekta ya ushirika nchini._*

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Hassan Wakasuvi kutokana na mchango wake mkubwa katika shughuli za maendeleo nchini.

Amesema hayo leo (Jumamosi Februari 24, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maziko ya Ndugu Wakasuvi yaliyofanyika katika kijiji cha Mabama mkoani Tabora.

Amesema kuwa Ndugu Wakasuvi alikuwa kiongozi imara katika kusimamia shughuli za maendeleo ikiwemo sekta ushirika nchini na umahiri wake uliwezesha kuimarika kwa sekta hiyo na kuleta tija nchini. “Aliiwakilisha nchi vyema kwenye sekta ya ushirika sio Tanzania tu, bali Afrika Mashariki, Ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Afrika kwa ujumla. ”

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi amesema Ndugu Wakasuvi alikuwa na kiwango kikubwa cha kuaminika.

Ameongeza kuwa Ndugu Wakasuvi alikuwa kinara katika kuchochea umoja ndani ya CCM pamoja na maendeleo ndani ya nchi. Leo “Chama, Serikali na Wananchi tumepoteza kiongozi mahiri, tumuenzi kwa kuendeleza umoja na mshikamano.”

Previous articleWAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA MAZISHI YA COMRED WAKASUYI TABORA
Next articleRAIS DKT. SAMIA AHUDHURIA MAZISHI YA HAYATI RAIS DKT. HAGE GEINGOB WA NAMIBIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here