Home BUSINESS MRADI USAID ‘TUHIFADHI MALIASILI’ WANUFAISHA SHOROBA.

MRADI USAID ‘TUHIFADHI MALIASILI’ WANUFAISHA SHOROBA.

Mkurugenzi Mkuu wa JET, John Chikomo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku mbili kuhusu shoroba, uhifadhi na mazingira wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

 

 

Dk Elikana Kalumanga Ngallaba kutoka RTI International ambaye ni meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili akitoa mada kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa waandishi wa habari za mazingira na uhifadhi.

Ofisa Uhifadhi wa TFS Ruben Magandi akifafanua jambo kuhusu TFS inavyoshiriki kuhifadhi misitu na mazingira kwa waandishi wa habari wa habari za mazingira na uhifadhi.

Na Selemani Msuya

MIAKA miwili ya utekelezaji wa Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unaotekelezwa katika shoroba saba imetajwa kuwa na mafanikio makubwa katika maeneo husika.

Hayo yamesemwa na Dk Elikana Kalumanga kutoka RTI International ambaye ni Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari za mazingira na uhifadhi ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET).

Meneja huyo amesema mradi huo wa miaka mitano unaohusisha shoroba saba kati 61 zilizoanishwa na Serikali umepokelewa vizuri na wada wakiwemo wananchi, sekta binafsi na serikali, hali ambayo imesabanisha kuwepo kwa ufanisi na matokeo chanya kwa haraka.

“Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unatekelezwa katika shoroba saba ambazo ni Kwakuchinja inayohusua Tarangire na Manyara, Msitu wa Amani na Nilo, Udzungwa na Hifadhi ya Nyerere, Ruaha Rungwa na Katavi, Ruaha Rungwa na Inyonga na Kigosi Moyowosi- Burigi Chato,” amesema.

Meneja huyo amesema kupitia utekelezwaji wa mradi huo, kumekuwepo na mwamko mpya kwa wadau wengine kuelekeza nguvu kwenye shoroba zingine, jambo ambalo litawezesha kuziokoa.

Amesema shoroba nyingi zimathiriwa na shughuli za kibinadamu kwa muda, hivyo ni wazi mwamko ulipo sasa utaenda kuziokoa na kuwa salama.

Dk Kalumanga amesema ni vema jamii ikatambua kuwa faida ya kutunza shoroba sio kwa ajili ya wanyamapori, bali sekta nyingine mtambuka kama uwekezaji kwenye utalii na nyinginezo.

“Shoroba zina fursa nyingi tofauti na mapito ya wanyamapori, hivyo tunapaswa kuzitunza ili zichangie uchumi na maendeleo,” amesema.

Aidha, Kalumanga amesema pia mradi huo umeangalia eneo la mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa na athari kubwa katika baadhi ya maeneo, hali ambayo inachangia mwingiliano wa wanyama na binadamu kuongezea kutokana na kutafuta mahitaji, hivyo migogoro kuongezeka.

Amesema iwapo kila mdau atashiriki kuhifadhi shoroba ni wazi kuwa udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi utafanikiwa kwa urahisi.

“Tumeweka mkazo pia kwenye kupambana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo kuhifadhi misitu na kupanda miti mipya ambayo itawezesha kukabiliana, huku tukihakikisha wananchi wanafaidika kwa sasa na vizazi vijavyo,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS), Ruben Magandi amesema wamekuwa wakishiriki kutunza na kuendeleza shoroba hasa kwa kuhamasisha upandaji miti.

“Sisi tunashirikiana na taasisi zingine za kisheria na za usimamizi wa maliasili zilizopo kwenye shoroba mbalimbali na tumeona mwamko ni mkubwa kwa jamii kushiriki,” amesema.

Magandi amesema ili kuhakikisha shoroba zinakuwa endelevu ni jukumu la kila mdau kulinda na kuhifadhi mimea ambayo ipo hatarini kutoweka.

Ofisa huyo alitaja mimea ambayo ipo hatarini kutoweka ni Mpingo, Msandali na Mkurungu ambayo ina mchango mkubwa katika uhifadhi na mazingira.

Magandi amewataka wadau wote wa uhifadhi kushiriki kutunza misitu na kupanda miti ya asili na matunda kwenye maeneo yao ili kujiongezea kipato.

Aidha, Magandi ameainisha changamoto ambayo wanakutana nayo katika uhifadhi ni baadhi ya watu kuvamia misitu kwa ajili ya kilimo, kukata mikaa na shughuli nyingine kinyume cha sheria.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa JET, John Chikomo amesema jitihada zao ni kuhakikisha waandishi wa habari wanatumia kalamu na vipaji vyao kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida ya kutunza na kulinda shoroba na misitu.

Chikomo amesema JET kwa kushirikiana wadau mbalimbali ikiwemo RTI wanaosimia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili wamekuwa wakitaribu mafunzo na kuwezesha waandishi kwenda kuona na kuandika habari za uhifadhi wa shoroba ambapo matokeo yake yamekuwa mazuri.

“Huu ni mwaka wa tatu wa utekelezaji wa mradi, tulianza 25, ila tumekuwa tukipunguzana, lengo ni kuhakikisha tunapata waandishi wenye nia ya dhati ya kuandika habari za shoroba, uhifadhi na mazingira, kusema kweli nyie mliopo hapa mmefanya vizuri nawaomba muendelee kutetea sekta hii ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,” amesema.

Amesema JET haipo tayari kubeba mtu ambaye hafanyi kazi na kwamba lengo lao ni kuona sekta hii inaleta mabadilijko chanya kwa jamii na nchi kwa ujumla.

Mwisho

Previous articleTEGETA ‘A’ HADI MADALE WAITWA MAUNGANISHO HUDUMA YA MAJI
Next articleNEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO MAJIMBO 23 YA TANZANIA BARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here