Home LOCAL WANANCHI SONGEA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MENEJA WA TANROADS MKOA WA...

WANANCHI SONGEA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MENEJA WA TANROADS MKOA WA RUVUMA

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa meneja wa Tanroads mkoani Ruvuma Mhandisi Felix Ngaile aliyefariki wakati akishiriki mbio za kuchangia mahitaji ya watoto njiti katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma(Homso)

Na Mwandishi wetu Ruvuma

Wakazi wa Manispaa ya Songea,wamejitokeza  kuuaga  mwili wa  aliyekuwa Meneja wa wakala wa Barabara( Tanroads )Mkoa wa Ruvuma  Mhandisi Mlima  Felix  Ngaile( 55)  aliyefariki ghafla juzi.

Marehemu Felix Ngaile ,alipatwa  na  mshituko wa moyo wakati akikikimbia Mbio za hisani  za km 5 zilizoandaliwa na  Shirika lilisilo la kiserikali la Wiloles Foundation  kwa ajili ya kuchagia fedha za kununua  vifaa tiba ili kuokoa maisha ya watoto  waliozaliwa kabla ya muda (Njiti)

Akiongoza  waombolezaji walijitokeza kwa wingi kwenye ibada iliyofanyika  kanisa katoriki jimbo kuu la songea,Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman  Kapenjama Ndile aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Kanali Laban Thomas    alisema,Marehemu  amefariki kutokana na mshituko wa moyo (BP) .

Mkuu wa Wilaya Kapenjama Ndile alisema, kwamba  pamoja  na dhamila yake kubwa ya kuchangia  watoto Njiti  wa mkoa wa Ruvuma , alipatwa na mauti  wakati akitimiza adhima ya kuhakikisha anashiriki  mbio za hisani kama alivyokuwa ameahidi kwa waandaaji .

 “kifo  kinaukatili sana,kwasababu namna kinavyoondoa ndugu zetu  wapo wanaoondoka ghafla kama mhandisi  Ngaile , na wapo wanaougua  na kulazwa hospitali  na kuzidi kupoteza matumaini  na baadaye taarifa za kifo zinapotokea tunasema ameteseka sana acha apumzike, hatusemi  kifo kama hicho hakiuzunishi , tofauti na hiki kinachotokea ghafla kinaumiza zaidi  ,”alisema Mkuu huyo wa Wilaya Kapenjama Ndile.

Aidha ,amewataka wananchi kuacha maneno  kuwa Kuna hujuma imefanyika  bali Mungu pekee ndiye anayejua na wauchukulie msiba huo kuwa ni wa kawaida
Wapo watakufa wakiwa safarini, kazini ,nyumbani  ,hospitali na hata nyumba za wageni .

Pia Ibanda hiyo imehudhriwa na viongozi mbali mbali wa Chama na serikali , wananchi  wakandarasi,watumishi wa taasisa na idara za serikali wakiwemo watumishi wa  Tanroads  mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na mkuu wa kitengo cha matengenezo Mhandisi Roman Mbukwini.

Akiongoza Ibada hiyo Paroko wa jimbo kuu Songea  Padri Daniel Oteno,  amewataka waumini kutambua kuwa maisha ni mtihani,hivyo wanapaswa kujiandaa  na endepo Mhandisi Felix angejua kuwa kwenye mazoezi yake ndio ingekuwa mwisho wake angewaaga marafiki zake kuwa hatorudi lakini tutambue maisha ni kama maua asubuhi yana chanua jioni yananyaukaa.

Padre Oteno, amewataka watumishi kwenye nafasi zao kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja  na    kujenga tabia ya kumtegemea Mungu kwenye kila kitu wanachofanya ikiwa ni pamoja na kusali  zaidi ili kujiandaa kwani Maisha  ni mtihani tujiandae ,na kwamba Wafanyakazi  wachukue  kazi zao kama daraja la kwenda Mbinguni na siyo kutumia kazi zao kama mwisho wao na ,wafanye kazi zao kwa kutengeneza  barabara  kwa ajili  utukufu wa kwenda mbinguni.

” kila mmoja kwa nafasi yake asijisahau katika msiba  huu wa felix  tuwe na sara , sara ya kwanza  ya Yesu Ee bwana Mikononi mwako naiweka Roho yangu , hakuna zawadi sasa hivi kwa Felix kama sara hii , haya ni maneno  ya Mbinguni ya utukufu , na kwa wale wote mtakao safiri kwenda Shinyanga sara hii msiiache “Alisema Padri Otieno.

Akisoma wasifu wa Marehemu  Meneja wa Tanroads Mkoa wa Songwe ,Suleiman  Bishanga  ambaye aliwawakilisha Mameneja wa Tanroads nchini  alisema, marehemu Ngaile alizaliwa  Novemba 9,1968 amebahatika kufanya kazi katika mikoa mbali mbali ikiwemo Mwanza, Mara, kilimanjaro na  hadi anapatwa mauti alikuwa ni Meneja wa Mkoa wa Ruvuma  ambapo alilipoti Oktoba 2023  na  ameacha mjane na watoto  watatu , atakumbukwa kwa uhodari wake na pengo lake ni gumu kuzibika. .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakandarasi  Mkoa wa Ruvuma,  Charles  Mhagama amesema amepokea kifo hicho kwa uchungu mkubwa wanamuachia Mungu kwani alikuwa msaada kwa wakandarasi  na alitatua kero zao kwa wakati muhafaka.

“Kifo Sawa na mtego ni vema kucheki afya mara kwa mara na tutende mema kama ambavyo  marehemu alikuwa akifanya ili hata muda wa kuondoka duniani ukifika tukumbukwe kwa mema kama Mhandisi Ngaile,”alisema Mhagama.

Mhandisi  Roman Mbukwini Msimamizi wa kitengo cha Matengenezo wa wakala wa barabara(Tanroads)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Roman Mbukwini alisema,kiongozi ambaye alikuwa kama Baba kwa watumishi wa chini yake kwani alipenda sana kuwashirikisha na kuwafundisha kazi.

“Alikuwa ni zaidi ya mwalimu, zaidi ya baba na kiongozi  kwa watumishi  wenzake”

Aidha Mbukwini,amewashauri wati  wanapoandaa mashindano ya riadha yanayowashirikisha watu wa rika na umri tofauti ni vema kwanza wawapime watu afya zao kabla ya kuanza mashindano ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here