Home LOCAL UN WOMEN’S YATOA MAPENDEKEZO YAKE YA MISWADA YA UCHAGUZI NA VYAMA VYA...

UN WOMEN’S YATOA MAPENDEKEZO YAKE YA MISWADA YA UCHAGUZI NA VYAMA VYA SIASA 2023 KWA MLENGO WA JINSIA

Mwezeshaji na Mtaalam Kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania, aliyeongoza kuandaa miswada mitatu ya uchaguzi na vyama vya siasa, 2023 katika mlengo wa Kijinsia. Dkt. Victoria Lihiru, akitoa mada juu ya uchambuzi na mapendekezo ya miswada hiyo kwa Wahariri wa Habari, katika Kikao kazi kilichoandaliwa na UN WOMEN’S chini ya Mradi wa ‘Wanawake Wanaweza’ mradi wa Uongozi na Haki za Kiuchumi kwa Wanawake, mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkaazi nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UN WOMEN’S), Hodan Addou, akizungumza alipokuwa akifungua rasmi kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Shirika hilo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati Tendani, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena (kushoto), akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodaus Balile, katika kikao hicho.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake UN-WOMENS, limetoa mapendekezo yake kupitia miswada mitatu ya uchaguzi na vyama vya siasa, 2023 katika mlengo wa Kijinsia.

Miswada hiyo ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya masuala yanayohusu Vyama vya Siasa na Gharama za uchunguzi, pamoja na Muswada wa Sheria ya Uchunguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Akizungumza katika kikao kazi kati ya UN WOMEN’S na Wahariri wa Habari nchini kilichofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji na mtaalam Kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania, aliyeongoza kuandaa miswada hiyo Dkt. Victoria Lihiru, amesema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa vyama vya siasa vikaelekezwa kuwepo kwa uwiano wa asilimia 50 ya viongozi wake katika ngazi zote.

“Kumekuwa na uhaba mkubwa wa wanawake wanaogombea katika nafasi mbalimbali za Uchaguzi.

“Tunapendekeza kuwepo na asilimia au idadi kadhaa ya wagombea katika ngazi za uongozi na kuhakikisha kwamba wanawake wanakwenda kwenye Majimbo, Kata na Mataa kugombea nafasi hizo.

“Hivyo vyama vinapaswa kuhakikisha kunakuwepo na uwiano wa 50 kwa 50 wa wanawake wanaogombea” amesema Dkt. Lihiru.

Aidha miswada hiyo imegusia kushughulikia suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, nakwamba wamependekeza kuwepo kwa adhabu ya shilingi Milioni 5 hadi 1 wakati wa uchaguzi, lugha ya matusi, ukatili wa kingono na kejeli dhidi ya wagombea wanawake.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendani, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodaus Balile, amelipongeza Shirika la UN WOMEN’S kwa kuandaa mapendekezo hayo yatakayokwenda kuboresha na kuongeza tija katika miswada hiyo, huku akishauri kuwepo na mtazamo wa jinsia zote kwa kuzingatia makundi yote katika jamii.

“Mapendekezo ni mazuri, lakini pia kuwepo na Mipango ya mtazamo wa jinsia zote kwa kuzingatia makundi yote katika jamii, yakiwemo vijana na watu wenye ulemavu” amesema Meena.

Mapendekezo hayo ya UN WOMEN’S yanaunga mkono jitihada za miaka mingi za wadau mbalimbali wa kutetea haki za Binaadam, haki za wanawake na usawa wa kijinsia, ambao wamekuwa wakipigania ushiriki sawa wa wanawake katika chaguzi, Siasa na vyombo vya kutoa maamuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here