Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AWASILI USWISI KUSHIRIKI MKUTANO WA WEF

MAKAMU WA RAIS AWASILI USWISI KUSHIRIKI MKUTANO WA WEF

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zurich nchini Uswisi. Tarehe 14 Januari 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 14 Januari 2024 amewasili nchini Uswisi ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) utakaofanyika tarehe 15 hadi 19 Januari 2024 katika mji wa Davos.

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya uchumi na uwekezaji, utawala bora, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kilimo. Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais atafanya mazungumzo ya uwili na viongozi wa mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa hayo.

Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.

Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu wa Rais – Habari

  

Previous articleUN WOMEN’S YATOA MAPENDEKEZO YAKE YA MISWADA YA UCHAGUZI NA VYAMA VYA SIASA 2023 KWA MLENGO WA JINSIA
Next articleMKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA ANGOLA WAANZA ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here