Home LOCAL TANZANIA YAWA MWENYEJI MASHINDANO YA BINTI AFRIKA KWA MARA YA KWANZA

TANZANIA YAWA MWENYEJI MASHINDANO YA BINTI AFRIKA KWA MARA YA KWANZA

Mkurugenzi Mtendaji wa KL International Agency, Alphonce Mkama Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kutangaza eneo litakalofanyika shindano hiloTanzania yawa mwenyeji, mashindano ya binti Afrika kwa mara ya kwanza

Na.Neema Mathew 

Nchi ya Tanzania inakwenda kushuhudia mashindano ya binti Afrika kwa mara ya kwanza yenye lengo kubwa la kuiambia Tanzania na Afrika nzima kuwa hapa ndipo itakapowekwa kambi ya binti Afrika, mashindano ambayo yanakuja kukuza lugha ya Kiswahili yanakuja kutangaza utu wa Mwafrika lakini pia ni mashindano ambayo yanakuja kuwaambia mabinti kutokujikondesha na kuwa na miili yao ya asili.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari, 6,2024, Mkurugenzi Mtendaji wa KL International Agency Alphonce Mkama, amesema kuwa mashindano hayo yanakuja kukuza lugha ya Kiswahili,kutangaza utu wa Mwafrika lakini pia ni mashindano ambayo yanakuja kuwaambia mabinti wa Kiafrika kutokujikondesha na kuwa na miili yao ya asili.

“Katika kuungana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa zaidi na sisi kupitia Binti Afrika tunakwenda kutangaza lugha ya Kiswahili na Eneo hili la Kingazi Tanzania ndio itakuwa kambi yetu kubwa na ndio ukumbi ambao utatumika kwa kila jambo ikiwemo kutembea kwa mikogo na maringo kwa mabinti hao

“Tunahutaji mabinti mabinti wenye maumbo makubwa na wenye nywele za asili na wenye ngozi ya asili wasiojichubua na mashindano haya yatashirikisha Nchi zote za Afrika na wiki ijayo tutatangaza mawakala kwa Nchi zote mpaka Sasa Nchi 30 zimeshathibitisha kushiriki.

“Kambi itachukua miezi minne ili kutoa fursa kwa wageni kufundishwa lugha ya Kiswahili kupitia wakufunzi mbalimbali kutoa vyuo vyetu vikuu,Bakita na Bakiza kuja kukutana na washiriki wetu kuja kuwafunza maneno mazuri ya kuvutia ya lugha ya Kiswahili,amesema Mkama.

Mkurugenzi Mtendaji wa KL International Agency Alphonce Mkama na Mkurugenzi wa Hoteli ya Kingazi, Nelson Mahenge wakionyesha mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja

Nae Mkurugenzi wa Hoteli Kingazi Nelson Mahenge amesema wamejiandaa kupokea ugeni mkubwa kutoka Nchi mbalimbali za Afrika na kuahidi kutoa huduma Bora zaidi

“Sisi tunapatikana maeneo ya Kijichi, Mgeni nani na nawakaribisha wageni na tupo tayari kuupokea ugeni huo,hapa tuna kila kitu ikiwemo malazi,chakula na vinywaji hivyo ukifika huduma zote zinapatikana nawaombea kila la heri washiriki wote ambao watakwenda kushiriki katika mashindano hayo, amesema,”Mahenge

Previous articleJIWE LA MSINGI SOKO LA MWANAKWEREKWE
Next articleBOMBA LA MAFUTA EACOP LATOA MIFUKO 1,000 YA SARUJI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here