Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa salamu fupi katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria Sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.
Picha zikionesha askari mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Amani tarehe 12 Januari,2024.