Timu ya Taifa ya Mali imeibuka kidedea kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Afrika Kusini katika mchezo wa kundi E wa michuano ya AFCON inayopigwa nchini Ivory Coast.
Mabao ya Mali yamepachikwa kambani na Nahodha wa timu hiyo Hamali Traole katika dakika ya 60 ya kipindi cha pili cha mchezo huo, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa nje kidogo ya 18 katika lango la Afrika Kusini.
Iliwachukua dakika 6 tu vijana wa Mali kupata bao la pili lilipachikwa kambani na Lassine Sinayoko katika dakika ya 66 ya mchezo huo.
Mtanange huo uliopigwa katika Dimba la Amadou Curibari ulianza kwa kasi kwa timu zote kucheza kwa nidhamu ya juu, huku Afrika ya Kusini ikicheza kwa kushambulia na kufanikiwa kupata mkwaju wa penati katika ya 19, ambapo Percy Tau alipaisha na kupoteza nafasi hiyo.
Kufuatia mchezo huo, Mali wameshika uongozi wa kundi E ikiwa na alama 3, ikifuatiwa na Namibia alama 3, huku Tunisia na Afrika Kusini wakiwa na alama 0.