Home SPORTS KOCHA TAIFA STARS ASIMAMISHWA

KOCHA TAIFA STARS ASIMAMISHWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemfungia mechi nane Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Adel Amrouche.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF, malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) dhidi ya Kocha Amrouche.

RMFF ilimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja n waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Kocha Adel Amrouche.

Kutokana na uamuzi huo, imemtea Hemed Morocco kuwa Kaim Kocha, na atasaidia na Juma Mgunda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here