Home BUSINESS Dkt. KIDA: SERIKALI IMEONDOA ONDOA TOZO ZAIDI YA 374 SEKTA YA UWEKEZAJI

Dkt. KIDA: SERIKALI IMEONDOA ONDOA TOZO ZAIDI YA 374 SEKTA YA UWEKEZAJI

Serikali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) umepunguza na kuondoa zaidi ya tozo 374 na kurekebisha zaidi ya sheria na kanuni 55 zinazowezesha Sekta binasfi kufanya kazi kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa Januari 22,2024 na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida, wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa BEGIN, uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kida amesema kuwa tozo zilizopunguzwa na Sheria zilizorekebiswa zimelenga Kuboresha Mazingira katika sekta za Uwekezaji, Kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, Utalii, Nishati, Madini, viwanda na Biashara

Aidha, Dkt. Kida amesema kuwa Mradi huo umelenga katika kukuza uchumi, kuongeza ajira na ubunifu kwa vijana na wanawake, kwa kuboresha mazingira ya Biashara, kuongeza usalama wa mlaji na kuwezesha wajasiriamali wakubwa, wa kati na wadogo kuzingatia ubora wa Bidhaa.

Amefafanua kuwa, Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), umetoa jumla ya Euro milioni 23 sawa na fedha za kitanzania Bilioni 63.5 ambazo zimeelekezwa kufadhili miradi mitatu ikiwemo Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) ambao awali ilikua ikijulikana kama BLUEPRINT.

Vilevile amefafanua kuwa fedha hizi zimelekezwa katika Mradi wa QUALITAN uliojikita umejikita kuimarisha maabara za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na UNDP katika mradi wa FUNGUO ambao umejielekeza katika kuwawezesha kampuni changa zinazochipukia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Cedric Medel amesema Kamati imejadili kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini na jinsi ya kusaidia kampuni zinazoibukia kukua na kuyafikia masoko.

Naye Mkuu anayesimamia Masuala ya UNIDO Bara la Afrika Bw. Victor Djemba wanaendelea kususisitiza wazalishaji kuzingatia ubora ili kufikia malengo yaliyowekwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here