Home BUSINESS WAZIRI WA FEDHA AIPONGEZA BRELA KWA HUDUMA BORA.

WAZIRI WA FEDHA AIPONGEZA BRELA KWA HUDUMA BORA.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba(Mb), ameipongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo leo tarehe 12 Desemba, 2023 wakati alipotembelea banda la BRELA lililopo nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), linapofanyika Kongamano la 14 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.

Dkt. Nchemba amesema amefurahishwa na huduma nzuri inayotolewa na BRELA ambayo ameilezea kuwa itaongeza idadi kubwa ya wadau watakaorasimisha biashara zao.

“Nimefurahishwa sana na huduma nzuri inayotolewa na BRELA, hivyo basi wafanyabiashara na wawekezaji ambao bado hawajarasimisha biashara zao ni vyema wakafuata taratibu sahihi za kusajili,” amesema Mhe. Dkt. Nchemba.

Aidha, Waziri wa Fedha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha, kuchangamkia fursa hiyo ya kurasimisha biashara zao na kufika katika banda la BRELA ili kupata huduma za urasimishaji.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa, Taasisi itaendelea kutoa huduma bora wakati wote, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wadau hawakumbani na vikwazo vya kibiashara.

Kongamano la 14 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lililofunguliwa leo tarehe 12 Decemba, 2023 litahitimishwa tarehe 14 Desemba, 2023 jijini Arusha.

Previous articleKINANA AZURU KABURI LA HAYATI RAIS MAGUFULI
Next articleHANDENI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA SARATANI 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here