Home LOCAL TMDA YAKAMATA WACHEPUSHAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA VYA SERIKALI

TMDA YAKAMATA WACHEPUSHAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA VYA SERIKALI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, (katika), Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari akitoa taarifa  ya Operesheni maalum ya kukamata Dawa, Vifaa Tiba tiba na Vtendanishi Bandia, duni na zisizosajiliwa uliofanyika leo Diesemba 20, 2023 Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, Akionesha kwa waandishi wa Habari moja ya Dawa bandia zilizokamatwa  kwenye Operesheni hiyo, kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Diesemba 20, 2023 Jijini Dar es salaam.

Msajiri wa Baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe, (kushoto), akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika leo Disemba 20, 2023, Katika Ofisi za TMDA Jijini Dar es Salaam.

Naibu Kamisha wa Jeshi la Polisi, CID Daniel Nyambabe, akizungumzia ushiriki wao katika Operesheni hiyo, iliyofanyika kwenye mikoa 13 ya nchini.

Na: Mwandishi wetu

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, amesema wamefanya Operesheni kabambe na kufanikiwa kunasa wachepushaji wa Dawa za Serikali huku ikionya wanaootengeneza, kusambaza, kuuza Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi bandia, kuacha mara moja kwani ni hatari kwa afya ya jamii.

Fimbo ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia kwenye mkutano na Waandishi wa habari akitoa taarifa  ya Operesheni hiyo, uliofanyika leo Diesemba 20, 2023,  Jijini Dar es salaam.

Katika Mkutano huo ametaja mikoa vinara kwa uchepushaji wa Dawa za Serikali ambavyo ni Dar es Salaam, Lindi na Simiyu.

Amesema kuwa Operesheni hiyo iliyofanyika tarehe 20 hadi 24, Novemba mwaka huu,  ilikuwa na lengo la kubaini na kuchukua hatua dhidi ya makosa ya ukiukwaji wa sheria ya Dawa na Vifaa Tiba  ya mwaka 2019 ikiwemo uwepo wa sehemu za Bashara za Dawa na Vifaa Tiba zinazoendeshwa bila kuwa na vibali kutoka mamlaka husika.

“Wilaya au mikoa husika ilichaguliwa kutokana na rekodi za matokeo ya miaka ya nyuma ya kaguzi mbalimbali za TMDA, na pia taarifa za kiintelijensia kutoka katika vyombo vya udhibiti,”.amesema Fimbo.

Ameongeza kuwa watoa huduma za afya kwenye Hospitali, vituo vya afya na zahanati za Serikali, kuacha kuiba Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi na kuuza kwenye Hospitali na maduka binafsi kwa lengo la kujipatia kipato kisicho halali, kwani hatua kali za kisheria zitachukulia kwa atakaefanya hivyo.

“Nayaelekeza Mabaraza ya kitaaluma, yaani Baraza la famasia na lile la mifugo, kufanya ukaguzi ili kuangalia kama wataalam wanasimamia maduka hayo,” amesema Fimbo.

Naye Msajiri wa Baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe amewataka wataalam wote wa afya kuwa na weredi  katika kununua dawa ili kuweza kulinda afya za wananchi.

Aidha Elizabeth amewataka pia kutoa taarifa katika maeneo yao lakini pia kutumia mfumo rasmi wa ununuzi wa dawa na kuacha kununua dawa mikononi.

“Wamiliki wote wa maduka ya dawa wanapaswa kununua dawa katika mfumo rasmi, dawa zilizosajiliwa lazima zipite kwenye mfumo rasmi, hizo zinazopita mikononi ni zile ambazo azijasajiliwa na ni hatari kwa afya ya binadamu” amesema

Katika ukaguzi huo uliohusisha mikoa 13 ikiwemo Dar ee salaam, Dodoma, Morogoro, kigoma, katavi, Mwanza, Simiyu,  Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Lindi na Ruvuma,  jumla ya majengo 777 yalikaguliwa ambapo kati yake 283 ni famasia, 23 maduka ya Vifaa Tiba , maghala ya dawa 9 ,na maghala 2  ya vifaa Tiba. Pia, kulifanyika ukaguzi wa maduka 105 ya dawa za mifugo,  maduka ya dawa muhimu za binadamu 272, (DLDM)30 vituo vya kutolea huduma za afya 30 , maabara 32, na kiwanda kimoja.

Operesheni hiyo ilifanywa kwa kushirikiana na TMDA, Ofisi ya Rais Mamlaka ya kupambana na Dawa za kulevyab(DCEA), Baraza la Femasia, TAMISEMI na Jeshi la Polisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here