Home LOCAL TASAF YAJENGA SHULE YA MSINGI YA (ENGLISH MEDIUM) KIJIJI CHA CHALOWE WANGING’OMBE...

TASAF YAJENGA SHULE YA MSINGI YA (ENGLISH MEDIUM) KIJIJI CHA CHALOWE WANGING’OMBE MKOANI NJOMBE

Mtendaji wa Kijiji cha Chalowe  Kata ya Igwachanya, Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe.  Bi. Felister Mwakifwamba, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari hawapo pichani waliokatika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF mkoani Njombe.

Sauli Enock Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa mradi wa TASAF CMC Kijiji cha Chilowe akifafanua baadhi ya Mambo kwa wahariri wa vyombo vya habari bands ya kutembelea mradi huo.

Moja ya jengo la madarasa katika shule hiyo Maya. 

………………………….. 

NA JOHN BUKUKU, NJOMBE

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umetoa shilingi milioni 268 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza inayojengwa katika kijiji cha Chalowe Kata ya Igwachanya, Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe.

Akizungumza  Desemba 21, 2023 katika Kijiji cha Chalowe, Kata ya Igwachanya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoa wa Njombe wakati wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa TASAF, Mtendaji wa Kijiji cha Chalowe Bi. Felister Mwakifwamba, amesema kuwa TASAF imetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha malengo yanafikiwa katika kukamilisha ujenzi wa Shule hiyo.

Bi. Mwakifwamba amesema kuwa wananchi wa Kijiji hicho wamechangia asilimia 10 kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za awali katika ujenzi wa Shule ikiwemo kuchimba msingi.

“TASAF wameleta fedha kwa ajili ya kuendeleza huu mradi, kwani wananchi tayari walianza kuibua kwa kuchimba msingi na vyoo” amesema Bi. Mwakifwamba.

Amesema kuwa katika Kijiji hicho wana miradi minne ikiwemo madarasa mawili na Ofisi moja, matundu ya vyoo sita, madarasa mawili na Ofisi moja ambayo yapo katika hatua ya mwisho ya umalinziaji.

Amefafanua kuwa mradi huo umekuja baada ya wanakijiji kuona hakuna shule ya mchapuo wa kiingereza ya serikali katika wilaya ya Wanging’ombe, hivyo uwepo wa shule hiyo itasaidia kuchochea maendeleo katika sekta ya elimu hasa kwa wazazi wemye kipato cha kawaida kusomesha watoto wao katika shule hiyo ambayo ni wazi gharama zake zitakuwa chini kuliko shule za binafsi

“Tunamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa shule hii kwani inakwenda kuleta tija kwa maendeleo ya kijiji chetu” amesema Bi. Mwakifwamba.

Baadhi ya wanakijiji cha Chalowe wameishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule.

“Kabla ya ujenzi wa mradi kuanza wanakijiji walipewa semina ya namna ya kusimamia mradi, tulianza ujenzi mwezi machi mwaka huu, wananchi wanafurai sana uwepo wa mradi huu, kama changamoto zikitatukiwa Januari Shule itafunguliwa” amesema wanakijiji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here