Home BUSINESS WAZIRI SILAA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WA VIJIJI, MITAA KUJIHUSIASHA NA UUZAJI WA...

WAZIRI SILAA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WA VIJIJI, MITAA KUJIHUSIASHA NA UUZAJI WA ARDHI

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amepiga marufuku Watendaji wa Serikali za Mitaa na Vijiji kote nchini kutojihusisha na Biashara ya uuzaji wa ardhi kwa wananchi.

Waziri Silaa ameyasema hayo katika kikao kazi na Wahariri na Waandishi wa Habari akitoa taarifa ya Utendaji kazi wa siku 100 za toka ateuliwa kuongoza wizara hiyo.

Kikao kazi hicho kimefanyika leo Disemba 22,2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi ya wananchi katika ununuzi wa Ardhi na kwamba viongozi hao wamekuwa wakihusishwa kwenye malalamiko kwa kuchukua asilimia 10 za wananchi kwenye Ardhi.

Amebainisha kuwa, Watendaji wa Serikali za Mitaa na Vijiji hawana Mamlaka ya Kisheria kufanya hivyo na kwamba kuanzia sasa masuala yote yanayohusiana na Ardhi yatafanywa na Maafisa Ardhi waliopo kwenye maeneo husika.

“Ninatoa maelekezo kuanzia leo, naagiza Watendaji wa Serikali za Mitaa waache Mara moja kujihusisha na masuala ya Ardhi, Waache kuchukua Asilimia 10 za Wananchi kwenye Ardhi, Maelekezo yangu ni kwamba Kuanzia leo masuala yote yanayohusu Ardhi yafanywe na Maofisa wa Ardhi waliopo kwenye eneo husika” amesema Silaa.

Katika hatua nyingine Waziri Silaa amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo kwenye mapitio ya Sera za Ardhi ili kuja na hatua ambazo zitaweza kumaliza changamoto ya Ardhi Ikiwemo migogoro ya Ardhi ambayo inawatesa wananchi kwa sasa.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa Waziri huyo katika kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha majukumu  yanayotekelezwa na Wizara yake yanaleta tija kwa Watanzania.

Previous articleTAASISI ZINAZOHUSIKA NA MRADI WA MAGADI SODA – ENGARUKA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUWEZESHA MRADI HUO KUANZA
Next articleTASAF YAJENGA SHULE YA MSINGI YA (ENGLISH MEDIUM) KIJIJI CHA CHALOWE WANGING’OMBE MKOANI NJOMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here