Home LOCAL SGR DAR MOROGORO KUANZA HUDUMA YA MAJARIBIO 2024

SGR DAR MOROGORO KUANZA HUDUMA YA MAJARIBIO 2024

Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema kuwa endapo majaribio ya reli ya SGR awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro yenye urefu wa kilomita 300 yakienda vizuri kufikia mwisho wa mwezi wa kwanza mwaka 2024 itaanza kutoa huduma ya majaribio kwenye awamu hiyo ya kwanza .

Akizungumza katika maonesho ya 16 wadau wa sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji, Waziri wa Uchukuzi Profesa, Makame Mbawara amesema kuwa kwa sasa serikalai inaendelea na majaribio ya awamu hiyo ya kwanza iliyokamilika kwa asilimia 98.65 yanafanyika kwa kutumia kichwa cha treni kinachokimbia spidibya kiwango cha kilomita 218.

Amesema kipande cha pili katika awamu ya kwanza ni kutoka Morogoro mpaka Makutupola ambapo kimekamilika kwa asilimia 95.7, Kipande cha tatu ni kitoka Makutupola mpaka Tabora kimekamilika kwa asilimia 12.2, Kipande cha nne ni kutoka Tabora mpka Isaka ambapo pia kimekamilika kwa asilimia 5.15 na kipande cha tano kwa awamu ya kwanza ni kutoka Mwanza mpaka Isaka ambapo kimekamilika kwa asilimia 44.22

Aidha Waziri Mabawara amesema serikali imefanya mabadiliko ya sheria ya reli namba 17 ambapo kwa sasa inaruhusu sekta zisizo za kiserikali kuja na vichwa vyao vya treni, mabehewa na kutumia mfumo wa relinya SGR jambo ambalo litaingizia taifa fedha na kukuza uchumi wa nchi huku akisema pia nia ya serikali ni kitoa fursa, huku akitoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

“Duniani kote saivi kuna kitu kinaitwa Open access- kufungua njia yako kama kuna watu wanataka kutumia njia yako kila mtu unampa muda wake kwa mfano kampuni A unampa muda utatumia njia kuanzia saa mbili mpaka saa tano, kampuni B unamwambia utatumia njia hiyo kuanzia saa sita mpaka saa nane ukifanya hivi unaitumia njia yako vizuri”, Amesema Waziri Mbawara.

” Mradi wowote una muda wa kuishi usipoutumia vizuri huwezi pata value of money”, Ameongeza Waziri Mbawara.

Maonesho ya 16 ya wadau wa Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji yanafanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa AICC jijini Arusha ambapo maonesho hayo yanahitimishea tarehe 8/12/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here