Home LOCAL SERIKALI YAINGIZA ZAIDI YA MILIONI 600, YATOA HATI MILIKI ZA ARDHI 3,156...

SERIKALI YAINGIZA ZAIDI YA MILIONI 600, YATOA HATI MILIKI ZA ARDHI 3,156 DODOMA

Na Eleuteri Mangi, WANMM

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na jiji la Dodoma imetoa Hati Miliki za ardhi 3,156 na kuwahudumia wananchi 7363 waliofika kwenye Kliniki ya Ardhi na kuongeza mapato ya Serikali zaidi ya Sh. Milioni 600.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda Desemba 12, 2023 wakati akitoa tathmini ya Kliniki ya ardhi iliyoendeshwa katika jijini Dodoma kuanzia Novemba 4, 2023 kutatua migogoro ya ardhi katika jiji hilo ili kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yambayo alielekeza Wizara kuhakikisha migogoro ya ardhi inapatiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri Pinda amesema katika zoezi hilo, jumla ya maombi mapya 2,433 ya umilikishaji wa ardhi yamepokelewa huku namba za malipo (control No) 8,539 zimetolewa na kuingizia Serikali kiasi cha Sh. 691,250,626.90.

“Zoezi hili ni mpango wa Wizara unaoendeshwa nchi nzima kweye ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri kwa lengo kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kutatua migogoro ya ardhi, kuwasogezea karibu wananchi huduma mbalimbali za sekta ya ardhi na kutoa elimu ya masuala yanayohusu ardhi” amesema Naibu Waziri Pinda.

Kwa upande wao wanufaika wa Kliniki hiyo Bw. Jerome Petro Mwenyekiti wa Mtaa wa Mahoma Makulu Kata ya Chawa na Bi. Asia Jabu Maalim kutoka Barabara ya 7 kata ya Madukani wamesema Kliniki hiyo imewasaidia wananchi wa Dodoma kwa kupata huduma kupata hati za viwanja vyao tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kliniki hiyo.

Aidha, wananchi hao wamepongeza uongozi wa Wizara na timu ya mkoa huo kwa kuwasogezea huma hiyo ndani ya jiji la Dodoma na kuwasaidia watu wengi kutatuliwa changamoto za migogoro ya ardhi katika maeneo yao.

Kwa kuzingatia umuhimu wa kutatua migogoro ya ardhi kwa wananchi, wakati wote wa zoezi hilo, viongozi wa Wizara kwa kushirikiana Uongozi wa Mkoa wa Dodoma.  

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here