Home BUSINESS SERIKALI YAFUTA MASHIRIKA 4 YA UMMA, YAUNGANISHA 16

SERIKALI YAFUTA MASHIRIKA 4 YA UMMA, YAUNGANISHA 16

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ametangaza rasmi kuzifuta taasisi za umma nne na kuziunganisha taasisi 16 lengo likiwa kuimarisha utendaji kazi wa mashirika ya umma ili yaweza kuendelea kutoa mchango katika maendeleo ya Taifa.

Akizungumza leo Disemba 15 Jijini Dar es salaam na Waandishi wa Habari Profesa Mkumbo amesema kufuatia hotuba ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aliyoitoa bungeni April 22 mwaka 2022 alielekeza kufanya mapitio na uchambuzi wa kina kwa mashirika ya umma ili yaweze kujiendesha kwa faida.

Amesema kwa muktadha huo serikali iliunda timu ya wataalam kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu utendaji wa mashirika hayo kwa lengo la kubainisha changamoto za kiutendaji na kupendekeza hatua za kuchukua katika kuongeza tija ya maendeleo nchini.

“Katika awamu ya kwanza serikali umeridhia na kuelekeza kuunganishwa kwa mashirika na taasisi 16 na kufuta mashirika na taasisi nne“amesema Profesa Mkumbo.

Taasisi na mashirika ya umma zilifutwa/ kuvunjwa.

Profesa Mkumbo ametaja mashirika na taasisi za Umma zinazofutwa/kuvunjwa ni pamoja na Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPFCS),Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC).

Pia Shirika la Elimu Kibaha (KEC) linavunjwa na kuunda Shule ya Sekondari Kibaha ama kwa jina ambalo Mamlaka husikazitaamua na Chuo Cha Ufundi.

Kwa uamuzi huu hospitali ya Tumbi Kibaha haitakuwa tena sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha bali hospitali ya Mkoa wa
Pwani na Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya,”ameongeza.

Aidha amesema Bodi ya Pareto inafutwa na shughuli zake zitahamishiwa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

Aidha Profesa Kitila amewatoa wasisi watumishi wote wa umma walio kwenye taasisi hizo kuwa hakuna mtumishi atakae poteza ajira yake maslahi yao yote yatalindwa na kuzingatiwa kwa kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Mwisho

  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here