Home LOCAL MIUJIZA YA NABII JACKSON YAIBUA MAZITO

MIUJIZA YA NABII JACKSON YAIBUA MAZITO

Miujiza Ya Nabii Jackson Ibrahim Kutoka Arusha Yaibua Mazito Dar, Umati Wafichuliwa Siri Zao

Nabii Ibrahim Jackson wa Kanisa la Power Of Perfection lililopo Mtaa wa Tanzanite Kwa Mrombo, Arusha ambaye kesho (Ijumaa) anahitimisha kongamano la maombezi na ufunuo kwenye kusanyiko lililopo Ukumbi wa Pemuha uliopo Gezaulole Dar, jana alifanya miujiza mikubwa ya uponyaji na kuwafungua waliofungwa na vifungo mbalimbali.
Wanahabari wetu walishuhudia maombezi ya Nabii huyo aliyekuwa akiwaponya watu kwa mafuta ya upako na maji yaliyobarikiwa na kufanywa kuwa damu ya Yesu.

Katika maombezi hayo, Nabii Jackson aliwatajia watu mbalimbali kwenye kongamano hilo maisha yao ya siku za nyuma na kuwatajia chanzo ya matatizo yao kilipoanzia ambapo wengi walionekana kukumbuka vyanzo hivyo na kukiri mbele ya nabii huyo kuwa alikuwa akisema ukweli kabisa ingawa wengi hawakujua kuwa hicho ndiyo kilikuwa chanzo.
Katika kongamano hilo walijitokeza watu walioingizwa kwenye uchawi bila ridhaa yao lakini wote hao aliwaangushia maombi na kuwapaka mafuta ya upako na damu ya Yesu na kuwatoa katika vifungo hivyo.


Akizungumza na wanahabari wetu nabii huyo alisema baada mkutano huo anarudi Arusha ambapo atapatikana kwa Mrombo Mtaa wa Tanzanite pia wanapatikana kwenye mitandao ya kijamii: facebook prophet jackson ministry, YouTube: Eden Tv, Tiktok:prophet jackson Ibrahim, namba za simu 0743758307 ambazo utaweza kuzungumza naye moja kwa moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here