Home LOCAL MAAFA HANANG: SERIKALI YAKESHA KUWEKA MIUNDOMBINU SAWA

MAAFA HANANG: SERIKALI YAKESHA KUWEKA MIUNDOMBINU SAWA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Kazi ya kuondoa tope katika Mji wa Kateshi Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara imeendelea kufanyika usiku na mchana ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mji huo unarejea katika hali yake ya awali baada ya kuharibiwa na maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ na kusababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali na miundombinu.