Home LOCAL HANDENI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA SARATANI 

HANDENI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA SARATANI 

Na: MWANDISHI WETU

WANANCHI wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wameendelea kujitokeza kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wa saratani mbalimbali ikiwemo ya mlango wa kizazi na matiti kwa wanawake pamoja na saratani ya tezi dume kwa wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Saratani ( OceanRoads) Dk. Maguha Stephano, alisema ni fahari kuoma wananchi wIlayani humo wanachangamkia fursa hiyo ya uchunguzi ugonjwa wa saratani.

Alisema ongezeko la wagonjwa wa saratani nchini ni tishio hivyo wataalamu wa Ocean Roads wameona haja ya kuinuka na kuifuata jamii kwa ajili ya uchunguzi wa awali.

Alisema, huduma hiyo inatolewa bila malipo, hivyo ni fursa kwa kila mwananchi kujitokeza na kutambua hali ya afya yake kwa upande wa saratani ili kuwawezesha kuanza matibabu wale watakaogundulika kuwa na tatizo.

“Walengwa wa huduma hii ni wananchi wote wenye dalili na wasio na dalili za magonjwa ya saratani, niwasihi wanaume kufika na kufanyiwa uchunguzi wa stezi dume unaofanyika kwa kutumia kipimo cha damu kama inavyofanyika kwa ugonjwa wa malaria,”alisema.

Alisema taasisi hiyo itaendelea kutoa huduma kupitia kampeni ya elimu na uchunguzi wa saratani inayoendelea kutolewa.

Dk. Maguha alisisitiza kuwa oparesheni hiyo ya upimaji wa saratani itafanyika katkka maeneo mbalimbali ikiwemo kituo cha afya Kituo cha Kideleko, Hospitali ya Wilaya Handeni Mjini, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,Mkata na kituo cha afya cha Kabuku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here