Home LOCAL WANANCHI WA ILEMELA WASIMAMISHA MSAFARA WA MAKONDA KUMPA PONGEZI ZA RAIS SAMIA,...

WANANCHI WA ILEMELA WASIMAMISHA MSAFARA WA MAKONDA KUMPA PONGEZI ZA RAIS SAMIA, ASIKILIZA KERO ZA STENDI YA MABASI YA NYAMUHONGORO

Wananchi, Wafanya biashara na Wadau mbalimbali Wilayani Ilemela wamesimamisha msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Cde. Paul Makonda kwa kumtaka kumpa salamu zao za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji kazi wake uliotukuka katika kutekeleza miradi mbalimbali Wilayani humo.

” Tunaendelea kumshukuru Rais Samia hakika ni Mama yetu kwani hakuna Mama anayeweza kumuacha mwanae, Mwanza tunaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo tunaomba umfikishie salamu zetu, pia tunakushukuru kwa kukuleta wewe , zamani nilikuwa nimezoea kukuita Mkuu wa Mkoa lakini kwasasa naomba nikuite Mkombozi wa Chama, Msaidie Rais wetu sababu wapo baadhi ya Viongozi hawafanyi kazi ni kama wamelala tuu_ ” Alisema mmoja katika wafanyabiashara wa stendi hiyo ya Nyamuhomongoro.

Mbali na hilo, wametoa kero na changamoto zao mbalimbali zinazowakumba katika ufanyaji wa shughuli zao za kiuchumi katika stendi hiyo ya Nyamongoro.

Previous articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 13,2023
Next articleFANYENI KAZI ZENYE MATOKEO CHANYA – DKT. BITEKO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here