Home LOCAL TUZO ZA WAKUU NA WATENDAJI WA MAKAMPUNI 100 BORA TANZANIA KUCHOCHEA UFANISI...

TUZO ZA WAKUU NA WATENDAJI WA MAKAMPUNI 100 BORA TANZANIA KUCHOCHEA UFANISI KAZINI.

Na Mwandishi wetu

TUZO za wakuu na watendaji wa makampuni 100 bora zaendelea kuwa chachu ya maendeleo Nchini kwa kuendelea kufanya kazi zaidi katika kuchochea ufanisi wa kazi.

Ukiwa ni msimu wa tatu wa Tuzo za wakuu na watendaji wa Kampuni 100 bora ‘Tanzania Top 100 Executive Awards” zenye lengo la kuwatambua watendaji wakuu wa makampuni mbalimbali wanaofanya vizuri Tanzania ili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Eastern Star Deogratius John Kilawe wakati wa utoaji wa Tuzo hizo Novemba 24, 2023 Jijini Dar es Salaam ambazo zilihudhuriwa na watendaji na wakuu wa makampuni mbalimbali Nchini.

Pamoja na mambo mengine Tuzo hizo zimelenga kutambua na kuthamini kile kinachofanywa na watendaji wa Makampuni Tanzania ikiwa ni moja kati ya Jitihada na harakati za kuchochea ukuaji wa Makampuni hayo na kuwatia moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuleta chachu ya maendeleo ya Sekta mbalimbali.

Kilawe amesema, wengi wamejitokeza na kushiriki katika Uzinduzi huo, pia ameongeza kuwa Uzinduzi wa Tuzo hizo hufanyika mara Moja Kwa mwaka na hutumika Ili kusheherekea na wakuu wa makampuni, mbinu za mafanikio kutoka kwa waliofanikiwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuonyesha njia za kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Amezitaja miongoni mwa sifa kuu za kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na Kampuni au mfanyabiashara kuwa na pato linaloanzia Shilingi Bilioni 1 na kuendelea na kuwa na hati safi za ukaguzi wa mahesabu ya kampuni kwa miaka mitatu iliyopita.

Ameongeza ya kwamba, kwa miaka 3 Sasa Eastern Star Grup imekuwa ikiratibu kwa Mafanikio tuzo hizo nchini Tanzania ambako wamekuwa wakifanya uchunguzi wa huduma mbalimbali za kibiashara na kuchangia ustawi, maendeleo na mafanikio ya kampuni shiriki na Taifa kwa ujumla.

“Tumefanya utafiti yakinifu na wa kina, ili kuwapata Wakuu na Watendaji wa Kampuni 100 bora nchini. Tunaamini kupitia mchakato huu utasaidia kutoa fursa kwa washiriki hao na kunufaika zaidi,” amesema.

Pia aliongeza kuwa Kwa kufanya hivi kunasaidia kuwatambua makampuni yanayofanya vizuri Tanzania kuendelea kuchochea fursa kwa Wawekezaji wa kimataifa kujitosa katika soko la Tanzania ili kuchochea zaidi Ukuaji wa Sekta mbalimbali nchini Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here