Home BUSINESS NSSF YATWAA TUZO YA USHINDI

NSSF YATWAA TUZO YA USHINDI

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetwaa Tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NSSF imepokea cheti na tuzo hiyo kwa kutambua utendaji kazi wa hali ya juu katika Wiki ya Huduma za Fedha.

Wiki ya huduma za fedha hufanyika kila mwaka na inaratibiwa na Wizara ya Fedha ikishirikisha wadau wa masuala ya fedha nchini, ambao ni wizara na taasisi za serikali, mabenki, makampuni ya bima pamoja na wadau wengine wa  serikali na sekta binafsi.

Kwa mwaka huu, Wiki ya Huduma za Fedha imefanyika jijini Arusha na ilianza tarehe 20 na inafikia tamati tarehe 25 Novemba 2023.

Previous articleTUZO ZA WAKUU NA WATENDAJI WA MAKAMPUNI 100 BORA TANZANIA KUCHOCHEA UFANISI KAZINI.
Next articleSIMBA YAKUBALI SARE 1 -1 DHIDI YA ASEC MIMOSAS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here