Home LOCAL MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) YAELEZA MPANGO KAZI NA UTEKELEZAJI WAKE

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) YAELEZA MPANGO KAZI NA UTEKELEZAJI WAKE

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali wa Elimu nchini na wananchi wote kujitokeza kuchangia mfuko wa Elimu Tanzania ili kushiriki katika maendeleo ya elimu hapa nchini.

Akizungumza katika kikao kazi kati ya Taasisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika mapema leo, Novemba 20, 2023 Jijini Dar_es _salam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Fabian, amesema kuwa Mamlaka ya hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kumtambua mtu  anayechangia elimu kupitia mfuko huo na kumuingiza kwenye Daftari la kudumu la wachangiaji.

Ameongeza kuwa pamoja na kutambuliwa katika Daftari hilo, pia atapata hati ya utambuzi kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha sheria ya mfuko wa elimu ya mwaka 2001.

“Mtu yeyote atakayeweza kuchangia elimu kupitia mfuko wa elimu atapata cheti ambacho anaweza kukipeleka kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitakachomsaidia kupata unafuu wa ulipaji kodi na sheria inaitaka mamlaka ya elimu Tanzania kujenga ushirikiano na Taasisi za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kushirikiana katika kuboresha elimu nchini,hivyo mamlaka inaushirikiano na taasisi mbalimbali kwenye kuchangia elimu na kuboresha elimu hapa nchini.

“Hili ni kati ya jukumu kuu la mamlaka ya elimu Tanzania katika kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo uandishi wa maandiko kwa ajili ya kupata wafadhili, kuendeleza mahusiano na taasisi mbalimbali zinazoweza kuchangia kwenye mfuko wa elimu”

“Pia Mamlaka inapokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi, watu binafsi na michango hiyo inaweza kuwa ya fedha au ya vifaa vikiwemo saruji, pamoja na mabati” amesema Fabian.

Previous articleBritam Insurance Tanzania yazindua mpango wa ufadhili wa masomo wakati inaadhimisha Miaka 25 katika soko la Tanzania
Next articleSOMA MAGAZETI LEO JUMANNE NOVEMBA 21-2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here