Home SPORTS SIMBA SC YASAINI MKATABA WA BILIONI 1.5 NA SBL

SIMBA SC YASAINI MKATABA WA BILIONI 1.5 NA SBL

Na: Neema Adrian

Dar-es-Salaam Klabu ya Simba kwa kushirikiana na kampuni ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager wamesaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya bilioni 1.5

Udhamini huo wa miaka miaka mitatu ambao thamani yake ni shilingi bilioni 1.5 utaifanya BIA yetu ya Pilsner Lager kuwa mdhamini wa Simba utakwenda kusaidia kukuza michezo,

Akizungumzia wakati wa utiaji saini leo Novemba 01, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries Limited, Obinna Anyalebechi amesema Udhamini huo utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni, Kwa udhamini huo wanaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba.

Kwetu sisi hii ni kubwa sana kwa sababu Simba Ina mashabiki wengi na inafanya vizuri hivyo basi tumeona kupitia Bia hii,ya Pilsner Lager tutakuwa tumekuza soka kwa kiasi kikubwa na soka letu liweze kwenda mbali zaidi,amesema Anyalebechi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa, Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana hivyo wamewashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba.

“Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili, Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka, Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira Nchini kwetu,” amesema.

Hata hivyo Meneja Masoko wa Bia za Serengeti Anitha Rwehumbiza amesema wanasimba kuwa wataanza kushiriki matukio ya Simba kwa kuanzia na derby na hata michezo za nje ya Dar, Kwao ilikuwa na ndoto lakini wanafuraha kwa kuwa tumekuja kwa muda sahihi watatumia watu, vyombo vya habari na watakuwepo uwanjani kuitangaza Pilsner Lager na Simba.

“Tulikuwa na lengo la kupata mshirika ambaye ana mashabiki wengi, na tulikuwa na furaha tulipopata taarifa kwamba Simba ipo tayari. Ukiacha kwamba Simba na Pilsner zinaendana kwa rangi na Simba pia Nguvu Moja ya Simba ni ya kuunganisha Watanzia wote na kinywaji chao cha Pilsner Lager.”amesema. Rwehumbiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here