Home LOCAL SERIKALI YAPELEKA VIFAA TIBA VYA MILIONI 900 IFAKARA

SERIKALI YAPELEKA VIFAA TIBA VYA MILIONI 900 IFAKARA

Na: MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 900 kwa Halmashauri ya Ifakara mji.

Akizungumza jana Mkoani humo Mbunge wa Kilombero Abubakar Asenga, alisema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia kuboresha huduma za afya hivyo wanaishukuru serikali kwa hatua kubwa ya maboresho katika sekta hiyo.

Alieleza kuwa, jimbo hilo lilikuwa na kero saba muhmu na kubwa ambazo hazijawahi kutatuliwa tangu kupata Uhuru lakini Rais Dk. Samia amezitatua ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara, maji, ukarabati kituo cha umeme Kidatu,ujenzi wa shule za kata, vituo vya afya, zahanati na hospitali.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya amesema ujio wa vifaa tiba hivyo ni neema kwa halmashauri hiyo.

Alisema, maboresho hayo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.Samia ni lazima kuungwa mkono na watendaji hivyo anatoa siku 15 kuhakikisha MSD inafunga vifaa hivyo na wananchi wanaanza kupata huduma.

“Niwaombe MSD ilete wataalamu wao kwa ajili ya kufunga vifaa hivi, haiwezekani Rais wetu afanye mambo makubwa kama haya watendaji tumuangushe, ni muhimu kuhakikisha tunasimamia na wananchi wanaanza kupata huduma kwa wakati,”alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa MSD ambaye ni Mfamasia na Afisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam Diana Kimario, alisema kanda hiyo ina hudumia mikoa mitatu ambayo ni Pwani, Morogoro na Zanzibar ambapo Ifakara ni mnufaika.

“Ujio wa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 900 ni muendelezo wa mabadiliko makubwa katika maboresho sekta ya afya, sisi watumishi ndani ya MSD tunajivunia namna serikali yetu chini ya Rais Dk. Samia na Mkurugenzi wa bohari Mavere Tukai wanavyohakikisha tunafanya kazi bila hofu.

Previous articleJWT YAANZA ZIARA PWANI
Next articleDIAMOND PLATNUMZ ASHINDA TUZO ZA MTV EMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here