Home LOCAL JWT YAANZA ZIARA PWANI

JWT YAANZA ZIARA PWANI

Na: Mwandishi Wetu, Pwani

JUMUIYA ya Wafanyabiasha nchini (JWT) imeanza ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wafanyabishara katika wilaya zote za mkoa wa Pwani.

Lengo la ziara hiyo ni kusikiliza kero za wafanyabishara, wenye viwanda na kampuni ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kuepuka changamoto ikiwamo migomo ya mara kwa mara.

Mwenyekiti wa JWT, Hamis Livembe, akiongozana na viongozi wengine mapema leo wamewasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kufanya mazunguzo na Katibu Tawala, Rashid Mchatta kabla ya kuanza mikutano yao.

Livembe amesema Rais Samia anawapenda wafanyabishara ndio sababu amewaagiza wasikilize kero zao ili kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Amesema wafanyabishara wakiungana wanaweza kujisemea na kumaliza kero zao bila kufunga biashara wala kufanya vurugu hivyo ni muhimu kujitokeza kwenye mikutano hiyo.

Naye Mchatta ameipongeza jumuiya hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuisaidia serikali kusikiliza kero hizo nchi nzima na kuzifilisha kwenye mamlaka husika.

“Niwasihi tu viongozi wa JWT msiache kuwaelimisha wafanyabishara umuhimu wa kulipa kodi pamoja hayo wazingatie tahadhari za mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini,” amesema.

Previous articleMAGAZETI YA LEO NOVEMBA 6-2023
Next articleSERIKALI YAPELEKA VIFAA TIBA VYA MILIONI 900 IFAKARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here