Home LOCAL KATIBU MKUU MADINI APONGEZWA

KATIBU MKUU MADINI APONGEZWA

Dodoma,

Watumishi wa Wizara ya Madini wa kada tatu tofauti za Makatibu mahsusi (PS), Watunza kumbukumbu na Wasaidizi wa ofisi wamemshukuru, kumpongeza na kumkabidhi zawadi ya saa na kishika funguo (Key Holder) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Kheri Abdul Mahimbali kutoka kuwafanikishia watumishi hao kwenda kushuhudia namna migodi inavyofanya kazi na kuwaongezea ushuhuda katika kufanikisha majukumu yao ambapo watumishi hao wametembelea migodi kadhaa ambapo jumla ya watumishi 27 wamefanya ziara hiyo ya kimkakati.

Mmoja wa watumishi hao Bi. Veneranda Charles amesema tangu alipoajiriwa wizarani humo mwaka 1994 (Miaka 29 iliyopita) hajawahi kutoka kwenda popote kujifunza lolote na ziara hii ya mwaka huu ni ya mara ya kwanza

“Mimi nina zaidi ya miaka 29 kazini kama muhudumu wa ofisi lakini hii ndio mara yangu ya kwanza kutoka na kwenda kujifunza shughuli za migodi japo kila siku nawahudumia watu wa sekta hii hapa ofisini” Ameshuhudia veneranda

Kwa upande katibu mkuu Mahimbali akipokea zawadi hizo amesema kwa anawashukuru kwa zawadi japo kuwa aliwaandalia ziara hizo ili wakajifunze ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ya kawaida

“Kwa kweli nawashukuru sana, mmenipa zawadi ya Saa kubwa ya ukutani na kidungua milango. Japo kuwa nilikuwa natimiza majukumu yangu ya kawaida lakini nawashukuru sana kwa kujali”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here