Home LOCAL Dkt. MWINYI AWASHUKURU UWT KUTHAMINI UONGOZI WAKE

Dkt. MWINYI AWASHUKURU UWT KUTHAMINI UONGOZI WAKE

Na:: Halfan Abdulkadir ZANZIBAR

Makamu Mwenyekiti wa  Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa yote ya Tanzania bara.

Dk.Mwinyi amesema hayo katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 04 Novemba 2023.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuimarisha umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.

Amesema katika miaka miwili iliyobaki utekelezaji wa miradi maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa.

Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar .

Vilevile ameeleza kuwa UWT watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar Dk.Mwinyi pia watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan mwaka 2025.

Previous articleMKEYENGE: TASAC HAIJAZUIA LESENI ZA KUSAFIRISHA KOROSHO NJE YA NCHI
Next articleRAIS DKT. SAMIA NA VIONGOZI WENZAKE KWENYE MKUTANO WA SADC ANGOLA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here