Home SPORTS Dkt. MWINYI AWAALIKA MABINGWA WA CECAFA U-15 IKULU ZANZIBAR

Dkt. MWINYI AWAALIKA MABINGWA WA CECAFA U-15 IKULU ZANZIBAR

Na: Halfan Abdulkadir -Zanzibar.

Dakika chache baada ya timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume boys) kutwaa ubingwa wa Cecafa U-15 huko Uganda, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Hussein Mwinyi amewapa mualiko wa kwenda Ikulu vijana hao watakaporudi Zanzibar.

Hii ikimaanisha kuwa Kiongozi huyo wa Nchi ameonyesha kufurahishwa na Vijana wa Timu hiyo.

Dokta Mwinyi amezungumza kauli hiyo wakati alipopigiwa simu na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo mbele ya Wadau mbali mbali wa Soka waliofika Kisonge Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kwa ajili ya kuangalia mpira ulikuwa unaoneshwa kwenye TV kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Leo Jioni November 16,2023 Karume boys imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga wenyeji Uganda kwa penalti 4-3 kufuatia dakika 90 kutoka sare ya 1-1, fainali iliyochezwa Uwanja wa Njeru huko Jinja Uganda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here