Home BUSINESS BoT YAWASISITIZIA WANANCHI UMUHIMU WA KUJIWEKEA AKIBA

BoT YAWASISITIZIA WANANCHI UMUHIMU WA KUJIWEKEA AKIBA

Afisa kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Usimamizi wa Huduma ndogo za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Deogratius Mnyamani akitoa elimu kwa wananchi. Mbalimbali waliotembelea katika banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha

(credit: Fullshangwe Blog)

NA JOHN BUKUKU, ARUSHA

Jamii imesisitiziwa umuhimu wa kuweka akiba, kuwekeza na kufanya matumizi kwa ajili ya mahitaji muhimu, kukopa sehemu rasmi pamoja na kuacha tabia ya kutumia fedha kwa ajili ya kutamani kitu kwani inarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi katika familia.

Akizungumza leo Novemba 23,2023 katika maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha yanayofanyika kwenye uwanja wa Sheilh Amri Abeid Jijini Arusha, Afisa kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Usimamizi wa Huduma ndogo za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Deogratius Mnyamani, amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakifanya matumizi kwa kutamani na sio kwa ajili ya mahitaji muhimu katika maisha.

Bw. Mnyamani amesema kuwa jamii inapaswa kutofautisha matumizi ya lazima na uasiyo ya lazima jambo ambalo litawasaidia kupiga hatua katika kufanya uwekezaji.

“Tunapaswa kujiuliza ni kweli nahitaji kufanya matumizi ya aina hii au nahitaji kununua simu ya bei kubwa au hii ya Sh. 30,000 inanifaa, tujenge tabia ya kuweka akiba kwanza kabla ya matumizi”amesema Bw. Mnyamani.

Amesema kuwa wakati umefika wa kuwa na utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili kusaidia kutatua dharula ya matatizo ya kifedha.

Amesema kuwa nchi za China, Japan na India zimefanikiwa kwa sababu wamekuwa na utamaduni wa kuweka akiba ya kutosha kuanzia ngazi ya familia na Taifa.

“Kuna hati fungani ambazo zinanunuliwa nchini Marekeni ni wachina na wajapani ndiyo wananunua na kufanya uwekezaji kutokana na kuwa na msingi mzuri katika masuala ya fedha” amesema Bw. Mnyamani.

Bw. Mnyamani amesema ili kufikia malengo wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kuhusu utoaji wa mikopo, kuweka akiba ya fedha pamoja na utunzaji wa fedha binafsi.

“Tunatoa elimu kwa wakinamama na vijana kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, watu wengi wanajua wanaoweka akiba ni matajiri jambo ambalo sio kweli” amesema Bw. Mnyamani.

Previous articleGAVANA TUTUBA ATEMBELEA BANDA LA BoT ARUSHA
Next articlePROFESA NDALICHAKO AANIKA UMUHIMU WA HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here