Home SPORTS TARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0

TARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0

Iringa

Timu ya Mpira wa miguu ya TARURA yaendeleza ubabe kwa siku tatu mfululizo ambapo Leo imefanikiwa kuipiga Ardhi goli 1-0 kwenye mashindano ya SHIMIWI.

Katika mchezo wa Leo uliochezwa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa,TARURA ilifanikiwa kuona goli la ardhi katika kipindi cha kwanza dakika ya 28 ambapo mchezaji Erick Tegamaisho aliipatia goli la ushindi.

Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Ardhi haikufanikiwa kuliona goli la TARURA licha la mchezaji wa TARURA Makunge Mwera kupewa kadi nyekundu.

Hadi Leo TARURA inaongoza kwa kuwa na point 9 na magoli 8 ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Wakili Mkuu iliibuka kidedea kwa magoli 4-0 na katika mechi ya pili dhidi ya Wizara ya Elimu ilitoka mshindi kwa 3-2.

Previous articleKIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA.
Next articleCOMRED MBETTO: KAZI ZA RAIS MWINYI KUIPA CCM USHINDI 2025
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here