Home LOCAL COMRED MBETTO: KAZI ZA RAIS MWINYI KUIPA CCM USHINDI 2025

COMRED MBETTO: KAZI ZA RAIS MWINYI KUIPA CCM USHINDI 2025

Na. Halfan Abdulkadir, ZANZIBAR.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Visiwani Zanzibar kimejigamba kushinda Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuendelea kuwaongoza Wazanzibari  kutokana na kazi kubwa inayoendelea kufanyika chini ya Rais Dk Hussein  Ali Mwinyi.

Kimeutaja  ushindi huo wa CCM  wa mwaka 2025 ni sawa na tetemeko lisilozuilika.

Hayo yamesemwa na Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi, Khamis Mbetto Khamis  ,wakati  alipofungua kongamano la Wanawake Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mbetto  aliwaeleza wanawake  walioshiriki kongamano hilo akiwaahidi  kuwa serikali ya CCM itaendelea kusimamia maslahi yote ya  wanawake, kupinga ubaguzi wa kijinsia na aina yoyote ya ukatili dhidi yao .

Alisema Wanawake wa CCM ni jeshi lenye mtaji wa ushindi hivyo hayupo atakayewapuuza katika harakati za kuelekekea maendeleo ya kweli ya Zanzibar na watu  wake. 

“Wanawake mtabaki kuwa ni sehemu ya maendeleo, hayupo anayeweza kuwaweka benchi na kuwasahau .  Kila mwanamke anathamani CCM tofauti na wale walioko upinzani .Nje ya CCM  wanawake hubaguliwi Wala kutengwa” Alisema Mbetto. 

Aidha Katibu huyo Mwenezi aliwanyooshea upande wa upinzani na kuutaka ufute ndoto za kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2025 Kisiwani humo .

‘Iwapo mwanasiasa kigogo Maalim  Seif Sharif  Hamad hakushinda waliobaki ni maharage ya mbeya.” Alisema kwa kujigamba.

Mbetto  alidai yuko Mwanasiasa mmoja wa upiinzani (hakumtaja jina) amedai  mwaka 2025 chama chao kisipotangazwa kimeshinda Uchaguzi ujao, Zanzibar  haitakalika  na kumjibu kwa kusema hawezi kufanya lolote na kuwataka Wananchi kuwa na amani kufanya mambo yao ya maendeleo.

Mkoa wa Kaskazini Pemba ni miongoni mwa maeneo yanayoaminika kuwa ni ngome ya Upinzani ambapo mara kadhaa imekuwa ikishuhudiwa mchuano mkali wa Kisiasa ndani ya Mkoa huo Kila ifikapo Uchaguzi.

Previous articleTARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU OCTOBA 2,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here