Home LOCAL NI MUHIMU KUCHUKUA TAHADHARI MAPEMA KUEPUKA MADHARA YA MVUA KUBWA

NI MUHIMU KUCHUKUA TAHADHARI MAPEMA KUEPUKA MADHARA YA MVUA KUBWA

Na: Elimu ya Afya kwa Umma.

Ikiwa Wizara ya Afya  imekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu juu ya tahadhari ya kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa baada ya Mamlaka ya Hali ya hewa kutangaza kuwepo kwa mvua za mafuriko , Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Shinyanga Flora Sagasaga amesema elimu hiyo ina faida kubwa kwa wananchi ambapo tayari ameshaanza kusisitiza wananchi kuhama mabondeni.

Sagasaga ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwalugulu  amebainisha hayo wakati akizungumza na Elimu ya Afya kwa Umma juu ya mikakati waliyoiweka kuhakikisha elimu inafika kila kitongoji katika Halmashauri hiyo.

“Tumeshasikia taarifa kuwa kutakuwa na mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wetu wa Shinyanga na sisi kama viongozi tumeshaanza kuchukua tahadhari, mimi katika kata yangu kati ya vijiji 6, vijiji 2 El nino ikiingia patakuwa na hatari vijiji hivyo ni Igudu na Mwankima watu wanaishi mabondeni sana hulima mpunga, tumeshaanza kuwaambia watoke mabondeni ili kuondoa madharaamesema.

Halikadhalika, Sagasaga ametumia fursa hiyo  kumpongeza Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu  kwa kuwa mstari wa mbele katika suala la uelimishaji katika kujikinga dhidi ya madhara ya mafuriko ikiwemo magonjwa ya mlipuko pamoja na  msisitizo kwa kamati za maafa kuimarishwa.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwemo Firiki Charles, Khadija Shaban Ng’hagala pamoja na pamoja Shija Lukenanga wamezungumzia umuhimu wa tahadhari ya mafuriko.

“Kama matangazo ambayo nimekuwa nikiyasikia kupitia vyombo vya Habari nasisitiza tu wazazi wenzangu tusiruhusu watoto kucheza karibu na kingo za maji, na vyombo vinavyosafiri visivuke maporomoko ya maji kwani si vyema kudharau nguvu ya majiamesema Firiki Charles.

Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania( TMA) imeshatangaza uwepo wa mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ikiwemo Shinyanga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mara, Kigoma, Morogoro, Pwani, Dar Es Salaam, Tanga, Arusha, Manyara na Kilimanjaro  ambapo Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma imekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuchukua tahadhari juu ya madhara yanayoweza kujitokeza.

MWISHO.

Previous articleGGML YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA MADINI GEITA
Next articleMKE WA PROF. JAY AIBUKA NA KIJIJI CHA NGURUWE DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here