Home BUSINESS GGML YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA MADINI GEITA

GGML YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA MADINI GEITA

Makamu wa Rais wa pili Zanzibar, Hemed Suleiman (kushoto) akimkabidhi tuzo Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika maonesho ya teknoloji ya madini Geita.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakifurahi tuzo walizozipata katika maonesho ya teknolojia ya madini Geita. GGML iliibuka na tuzo nne ikiwamo ya muoneshaji bora pamoja na mshindi wa jumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML,  Terry Strong (aliyevaa suti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaanyakazi wa GGML baada ya kuwaa tuzo nne katika maonesho ya teknojia ya madini Geita, ikiwamo mshindi wa jumla ya maonesho hayo ambayo pia GGML ilikuwa mdhamini mkuu.

NA: MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited imenyakua tuzo nne ikiwamo mshindi wa jumla katika maonesho ya teknolojia ya madini yaliyofanyika kwa muda wa siku 10 mjini Geita na kushirikisha washiriki zaidi ya 400.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza tarehe 20 Septemba hadi tarehe 30 Septemba mwaka huu, Hospitali ya rufaa ya mkoa Geita kwa kushirikiana na GGML, pia ilitoa huduma za upimaji wa saratani kwa wananchi zaidi ya 1000.

Akifunga maonesho hayo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman aliipongeza GGML pia kwa kuibuka na tuzo ya muoneshaji bora kwa mwaka 2023.

Kampuni hiyo pia ilipewa hati maalumu ya shukrani kwa kuwa mdau muhimu tangu kuanzishwa kwa maonesho hayo mwaka 2018 pamoja na hati ya shukrani ya kuwa mdhamini mkuu ambapo kwa mwaka huu ilitoa zaidi ya Sh milioni 150.

Akisoma hotuba hiyo kwa niaba ya Rais Samia katika maonesho hayo, Suleiman alisema Dira ya Sekta ya Madini (Vision 2030) inalenga kumaliza changamoto za muda mrefu kwa wachimbaji wadogo za kukosekana kwa taarifa za kuaminika za maeneo yenye rasilimali hiyo.

Dira ya ‘Madini ni Maisha na Utajiri’ imelenga kuhakikisha hadi kufikia 2030 utafiti wa madini kwa njia za jiofizikia uwe umefanyika nchini wa zaidi ya asilimia 50.

“Serikali inaendelea kuhakikisha wachimbaji wa madini wanapata masoko ya uhakika na itaendelea kuwawezesha wawekezaji wadogo wa sekta hii kwa kuwaunganisha na taasisi za fedha,” asema Rais Samia.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alisema katika siku 10 za maonesho hayo, anaamini washiriki wakiwa wachimbaji wadogo wamejionea na kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo GGML inazitumia katika kuhakikisha kuwa uchimbaji madini unafanyika kwa usalama na tija.

“Dhamira yetu ni kuongeza thamani kwa wadau wetu wote kuanzia shughuli za utafiti, uchimbaji na uchakataji wa dhahabu kwa kuongezea thamani na mambo mengine.

“Ni kwa sababu hiyohiyo kwamba tumefanya juhudi zote kuwezesha uhamishaji wa ujuzi na teknolojia kama inavyoonekana katika maendeleo ya miradi yetu mitatu ya uchimbaji na ushiriki wa wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma wazawa,” alisema.

Alisema GGML imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wazawa kupata mafunzo na zabuni za utoaji huduma ndani ya migodi ya kampuni hiyo kwa mujibu wa matakwa ya sheria ‘local content’ ambapo kwa mwaka 2015 kampuni hiyo ilitumia dola za Marekani milioni 202 na kiwango kimeongezeka hadi kufikia dolaza Marekani milioni 526 mwaka 2022.

Aidha, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia mbali na kuishukuru Serikali kwa kutambua jitihada za kampuni hiyo, alisema GGML itaendelea kutoa mafunzo kwa watanzania na wachimbaji wadogo ili waweze kupata fursa mbalimbali ndani ya mgodi huo.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema wanaamini ifikapo mwaka 2025 mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa utafikia asilimia 10.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OCTOBA 5-2023
Next articleNI MUHIMU KUCHUKUA TAHADHARI MAPEMA KUEPUKA MADHARA YA MVUA KUBWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here