Home KIDSNEWS MAHAFALI YA PILI SHULE YA AWALI NA MSINGI BECO YAFANA

MAHAFALI YA PILI SHULE YA AWALI NA MSINGI BECO YAFANA

Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog

Shule ya awali na msingi BECO iliyopo manispaa ya Shinyanga

Mkoani Shinyanga imefanya sherehe (mahafali) ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu darasa la

awali na darasa la saba mwaka 2023.

Sherehe hiyo ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu darasa la awali na

la saba imefanyika leo Oktoba 6, 2023 katika viwanja vya shule ya awali na

msingi BECO.

Akisoma historia fupi ya shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya

awali na msingi BECO Mwl. Lucas Mashimba amesema shule hiyo imekuwa na

mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ambapo mwaka 2021 shule hiyo ilishika nafasi ya 10 kitaifa kwenye matokeo ya

mtihani wa darasa la saba.

“Shule ya awali na msingi BECO ilianzishwa na kusajiliwa

rasmi na serikali mnamo mwaka 2018, kwa kufundisha kwa lugha ya Kiingereza

(English Medium), kwasasa shule yetu ina jumla ya wanafunzi 360 wavulana 176 na

wasichana 184 na kwenye mahafali haya ya pili ya shule hii tuna wahitimu 14

waliomaliza darasa la saba, 6 wakiwa ni wavulana na 8 wasichana.

Lakini pia

tunasheherekea mahafali haya tukiwa na wahitimu wa darasa la awali 30 wasichana

14 na wavulana 16 wanaotarajia kujiunga na darasa la kwanza mwaka ujao”,

amesema Mwl. Lucas Mashimba.

Kwa upande wake Mdhibiti ubora wa shule Aziza Yanga ameipongeza shule hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri kitaaluma na

kuwasihi wazazi na walezi kupeleka watoto kwenye shule zinazotambulika na

kusajiliwa ili kujihakikishia elimu bora inayotolewa kwa watoto wao.

“Palipo na dosari sisi kama wadhibiti ubora wa shule

hatupepesi macho lengo ni kujenga kizazi chenye elimu bora na si bora elimu,

wakazi wa Shinyanga tujivunie kwamba BECO PRE & PRIMARY SCHOOL ni miongoni

mwa shule bora hapa nchini”, amesema Aziza Yanga.

Mkurugenzi wa shule hiyo Machiya Ngelela  ameeleza malengo na

kipaumbele kikubwa cha shule hiyo kuwa ni taaluma bora hivyo anawakaribisha

wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika shule ya hiyo ili waweze kupata

elimu bora itakayowavusha kwenda ngazi nyingine kitaaluma.

Akizungumza kwa niaba ya aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe

mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Katibu Tawala wilaya ya shinyanga Said Kitinga

amewasihi wazazi kuendelea kuzingatia malezi kwa watoto wao pindi wawapo

nyumbani na kuwasihi wazazi wengine kupeleka watoto shuleni hapo

ili  wapate elimu bora katika shule ya msingi na awali BECO.

“Kwa kutambua mchango wa taasisi binafsi kwenye sekta ya

elimu, kwa uwepo wa shule ya awali na msingi BECO hapa Shinyanga inayokidhi

vigezo vya ufundishaji, wazazi naamini bado chaguo lenu ni shule ya BECO Pre

& Primary School kulingana na mazingira pamoja ubora wa elimu inayotolewa

katika shule hii kupitia waalimu na uongozi wa shule hii”, amesema Said

Kitinga.

“Mara baada ya watoto hawa kumaliza elimu ya darasa la saba

wawapo nyumbani tuendelee kuwafundisha kwa kusimamia maadili na miiko

yetu, lakini pia tuendelee kutoa taarifa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi

na usalama ili kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto”, ameongeza Said

Kitinga.

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akiwa kwenye mahafali hayo

Mwalimu Mkuu wa shule ya awali na msingi BECO Mwl. Lucas Mashimba akisoma taarifa fupi ya Shule hiyo.

Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi BECO , Machiya Ngelela akizungumza wakati wa mahafali ya shule hiyo.

Mthibiti Ubora wa Shule Aziza Yanga akizungumza wakati wa mahafali hayo.

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga Akizungumza wakati wa Mahafali ya shule hiyo



TAZAMA PICHA MBALIMBALI





Baadhi ya wazazi na walezi walioudhulia kwenye mahafali ya shule hiyo.

















Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akikabidhi vyeti kwa wanafunzi waliohitimu shuleni hapo,


Picha ya pamoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here