Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKIONGOZA MAPOKEZI YA KARDINALI RUGAMBWA

MAKAMU WA RAIS AKIONGOZA MAPOKEZI YA KARDINALI RUGAMBWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsalimiana na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya Kardinali Rugambwa kuwasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Vatican alipopewa hadhi ya Ukardinali Tarehe 06 Oktoba 2023).

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa pamoja na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa Mapokezi ya Kardinali Rugambwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Vatican alipopewa hadhi ya Ukardinali. (Tarehe 06 Oktoba 2023).

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya kumpokea alivyowasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Vatican. (Tarehe 06 Oktoba 2023).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa,Maaskofu pamoja na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa mapokezi ya Kardinali Rugambwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. (Tarehe 06 Oktoba 2023).

Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki mara baada ya kuwasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Vatican. (Tarehe 06 Oktoba 2023).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Askofu Gervas Nyaisonga,Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Accattino pamoja na viongozi wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa mapokezi ya Kardinali Rugwambwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Vatican. (Tarehe 06 Oktoba 2023).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa mara baada ya kumpokea nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Vatican. (Tarehe 06 Oktoba 2023)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea na kufanya kazi na kushirikiana vema na Kanisa Katoliki pamoja na madhehebu mengine ya dini hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa mapokezi ya Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Vatican alipopewa hadhi ya Ukardinali.

Amempongeza Kardinali Rugambwa kwa kuendelea kuhubiri amani na umoja wa Watanzania na kumsihi kuendelea kuwa chachu ya amani, upendo na umoja.

Makamu wa Rais amesema ni baraka kwa Taifa la Tanzania kupata Kardinali wa tatu.Kwa upande wake Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa amewaomba watanzania wa kila dini kuendelea kumuombea ili aweze kufanya vema kazi hiyo kwa uaminifu na kuweza kuleta maendeleo ya mwanadamu kwa ujumla kuanzia hapa nchini kimwili na kiroho na baadaye hata nje ya nchi.

Kardinali Rugambwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kanisa, Serikali na watanzania wote waliomtia moyo na kumtumia jumbe mbalimbali za pongezi zilizompa moyo na kumuimarisha.

Imetolewa naOfisi ya Makamu wa Rais06 Oktoba 2023Dar es salaam.

Previous articleMAHAFALI YA PILI SHULE YA AWALI NA MSINGI BECO YAFANA
Next articleMTENDAJI MKUU TARURA AWATAKA WATUMISHI BUHIGWE KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here