Home BUSINESS BRELA YAPIGA KAMBI MAONESHO YA EXPO S!TE 2023 JIJINI DAR KUTOA HUDUMA...

BRELA YAPIGA KAMBI MAONESHO YA EXPO S!TE 2023 JIJINI DAR KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakiwa tayari kutoa huduma katika Maonesho ya Swahili International Tourism Expo (SITE2023) kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Huduma zote za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma pamoja na utoaji wa Leseni za Biashara kundi “A”, Utoaji wa Leseni za Viwanda na Utoaji wa Hataza zitatolewa papo kwa papo katika banda la BRELA kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Oktoba, 2023.