Home BUSINESS WADAU SEKTA YA UVUVI WAMSHUKURU DKT.SEMIA KULETA AGRF TANZANIA

WADAU SEKTA YA UVUVI WAMSHUKURU DKT.SEMIA KULETA AGRF TANZANIA

Na David John

MKURUGENZI mtendaji wa Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavour limited kutoka mkoani Kigoma, Alpha Nondo amemmwagia pongezi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kuziweka pamoja nchi karibu 75 katika mkutano mkubwa wa kujadili mifumo ya chakula Afrika (AGRF) ambapo wao kama Kampuni inayoshughulika na uchakataji wa samaki wameweza kuhudhuria ili kuona fursa Bora ya soko.

Amesema wao ni wachakataji wa samaki kutoka ziwa Tanganyika ambapo ziwa hilo linasamaki adimu ambazo haziwezi kupatikana sehemu nyingine yeyote duniani.

Amesema wao kama Alpha wanahusika na samaki wa ziwa Tanganyika na wanafanya kazi na nchi za ulaya na samaki wake ni wazuri ukizingatia ziwa Tanganyika linasamaki ambao hawapatikani mahala pengine popote.

Mkurugenzi Nondo ameyasema haya leo Semptemba 4 ,2023 katika viwanja vya ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Saalam ambapo mkutano mkubwa wa chakula ulioshirikisha watu karibu 3000 unafanyika.

Amesema kuwa ziwa Tanganyika linatoa samaki wamapambo na wakila aina lakini wao wanachakata samaki wakiwemo wale wakitoweo na baada ya kuchakata samaki hao wanawapeleka nchi za Marekani, Canada ambapo wao kama Kampuni wanafanya kazi na umoja wa ulaya .

“Sisi tumekuja kwenye mkutano huu mkubwa ambao umeandaliwa hapa Tanzania Kwanza tunamshukuru mama Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa jitihada kubwa ambazo anafanya kama ndoto yake yakutaka Tanzania kuwa kitovu cha kulisha nchi zingine Afrika na Duniani na kwakweli tunaona jitihada zake Rais wetu .na ndio maana ameweza kuleta mkutano huu kwani anajua ili uwe kiongozi lazima uwe na elimu Kwa sababu elimu ni nguvu na ndio maana mama amesumbuka sana na kufanya jitihada za kufanya mkutano uje hapa Tanzania.

Nakuongeza kuwa ” Rais Dkt Samia anafanya hivi Kwa ajili ya manufaa ya watanzania kwanza hivyo lazima watu wajifunze namna ya kuwa kiongozi kwani kiongozi lazima uwe na elimu ya kujua namna gani unaweza kuongoza na kwakuleta mkutano huu anapenda tujifunze kutoka Kwa waliotangulia kwenye chakula na kubwa zaidi mtanzania anufaike.”Amesema Nondo

Ameongeza kuwa mkutano huo unafaida kubwa ambapo pia wageni wanaingia na wanakula ,kunywa, kulala, kupumua hewa ya Tanzania na watalala hoteli za Tanzania ,usafiri wa watanzania hivyo fursa ninyingi sana ambazo wanakwenda kufaidikanazo na hiyo ni jitihada ambayo mh Rais amefanya.

Nondo amefafanua kuwa wao kama wafanyabiashara ambao wanakwenda kuingia katika Soko la ushindani katika chakula wanakwenda kufaidika na njia mpya ambayo ndugu wageni wanakuja nayo namna Bora ya kuchakata chakula Ili kukidhi vigenzo vya huko nie na kwamba wakiwa na vigezo wakakubalika hakuna shaka uchumi utakuwa na hiyo ndio ndoto ya Rais Dkt.Samia na katika hapo hapendi hata mtanzania mmoja awe nyuma na mkutano huo ni Kwa ajili ya watanzania .

Nondo amesisitiza kuwa Kuna Kila sababu ya kuchangamkia na baada ya mkutano huo kumalizika basi wakae na kuona wapi wamepongeza ili kuboresha namna ya mkulima ,au mfugajo na kufanya namna ya kuchakata hadi kuandaa na kumfikia mlaji wa mwisho ili mwisho wa siku kukidhi vigenzo hiyo ndio lengo la rais na ndio maana wapi kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Amesema Kuna watu wametoka nchi mbalimbali wamekuja Tanzania na zaidi ya nchi 75 zimeweza kushiriki mkutano huo hiyo yote nijitihada ambazo Rais Dkt Samia.amefanya hivyo hawawezi kuacha fursa hiyo na wakabaki kama wanyonge lazima wasimame na kuchangamkia fursa hiyo hivyo watakaopata bahati ya kuja kwenye mkutano huo wasikae tu kuangalia mgeni.

Mkurugenzi Nondo ameongeza kuwa lazima watanzania wakae karibu na mgeni na kuweza kumuuliza anakotoka lengo nikupata mawili matatu kutoka kwake ikiwezekana wabadilishane hata mawasiliano.

“Mh Rais ameleta mkutano huu ili Kubadilisha mawazo ,tabia ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi na wao kama alpha mchango wao katika mkutano huu ni kwamba wameleta mashine Bora ya kisasa Kwa ajili kubania samaki ili kupata chakula Bora na hii ilitokana na huko nyuma Soko kutokubalika na ndio maana hata mkutano huu kwetu ni muhimu sana.sasa sisi tumetengeneza mashine hiii yenye uwezo wa kubanika samaki kama migebuka Kwa Tani mbili Kwa masaa sita hadi nane.Amesema Nondo.

Amesema kuwa wao hawatumii kuni na samaki hao wanachanganya na viungo ambavyo vinakwenda kuleta radha kwenye samaki hivyo imesaidia Kwa kiasi kikubwa kuleta soko na kutokana na ubanikaji huo wa kisasa wameweza kupata mataifa 22 ambayo wanazikubari ubora wake.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here