Home BUSINESS TANTRADE YAJIPANGA KUSAKA MASOKO YA BIDHAA ZA TANZANIA KIMATAIFA

TANTRADE YAJIPANGA KUSAKA MASOKO YA BIDHAA ZA TANZANIA KIMATAIFA

Na: Beatrice Sanga-MAELEZO

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema itaendelea kusimamia sera na miongozo mbalimbali ya kimaendeleo ili kuleta tija nchini kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo kuratibu Maonesho ya Biashara, misafara na mikutano ya wafanyabiashara, na kutafiti masoko mbalimbali kwaajili ya kukuza thamani ya bidhaa za ndani na kuongeza ushindani na bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa Septemba 4, 2023 na Latifa Khamis Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade wakati wa Mkutano wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mamlaka hiyo na wahariri wa Vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam huku akieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023, TanTrade imefanikiwa kuratibu matukio mbalimbali ikiwemo programu za utafiti, makongamano na misafara ya kibiashara, maonesho na mikutano ya kuunganisha wazalishaji na wanunuzi ambayo yameongeza makusanyo katika mfuko wa Hazina kwa asilimia 20.15 kwa kipindi cha miaka mitano.

Mkurgenzi huyo amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano, Tantrade ilifanikisha kusainiwa kwa jumla ya mikataba 46 yenye thamani ya Sh. 17.53 Trilion.

“Katika Kipindi cha miaka mitano (5) TanTrade ilipanga kukusanya jumla ya TZS 52,562,298,340 na imefanikiwa kukusanya TZS 40,004,650,548 sawa na asilimia 76, kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya mishahara na miradi ya maendeleo na vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo ada inayotozwa kwenye uratibu na usimamizi wa Maonesho, upangaji wakati usio wa Maonesho pamoja na ushiriki na viingilio vya Maonesho ya DITF.” Amesema Bi. Latifa

 Aidha Latifa amesema kuwa maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka yamezidi kuongeza thamani yake kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo kampuni za ndani na nje, washiriki, idadi ya nchi zilizoshiriki maonesho hayo, watembelea maonesho pamoja na ajira zilizozalishwa vimeongezeka na hivyo yamezidi kuongeza wigo wa biashara za ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo amesema kutokana na mafanikio hayo, “TanTrade imekamilisha maombi ya ufadhili ya kuendeleza rajamu (Branding) ya Taifa ya Viungo (Tanzania Spice Label) kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) pamoja na wadau wa sekta ya viungo, ambapo hadi Agosti, 2023 TanTrade imekamilisha rajamu ya iliki, tangawizi, mdalasini, pilipili manga na karafuu vilevile, Mamlaka inaendelea na taratibu za kukamilisha rajamu za bidhaa nyingine ikiwemo asali, korosho, kahawa na chai pamoja na mafunzo kwa wafanyabiashara 6,979 kupitia programu 26 ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha kiushindani.”

Aidha Tantrade imeendelea kusaka masoko nje ya nchi ya bidhaa mbalimbali zinazolishwa nchini ikiwemo mazao ya biashara na madini ili ziendelee kuongeza wigo wa uzalishwaji na kuongeza thamani ya mnyororo kwa wazalishaji lakini pia kuongeza fedha za kigeni ambapo mazao na madini hayo ni pamoja na Dhahabu, Korosho, Ufuta, Mbaazi, Kahawa, Dengu, Almasi, vifungashio vya mifuko, Pamba, mazao mengine ni Karafuu, Mchele, Soya, Karanga, Parachichi, Pilipili Muhogo, Mahindi, Karafuu, Asali, Mbegu Za Maboga, Korosho, Zabibu, Nyama.

“TanTrade imefanya uchambuzi wa takwimu katika mfumo wa ITC kutambua bidhaa zinazohitajika kwenye masoko mbalimbali duniani, Nchi ambazo zinahitaji bidhaa hizo ni pamoja na India, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uswisi, Vietnam, China, Pakistani, Japani, Marekani, Oman, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia.”

Mkurugenzi huyo ameongeza, “Kampuni ya Akros Cashew ya Tanzania imeuza Tani 37 za korosho zenye thamani ya Dola za Kimarekani 202,700 zimeuzwa kupitia Maonesho yaliyofanyika nchini Afrika Kusini, Kampuni za Tanzania zilifanikiwa kufanya mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 100,000 kwa bidhaa mbalimbali za kilimo na pembejeo kupitia msafara wa Malawi, Kampuni ziliweza kupata miadi ya mauzo yenye jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani milioni 20.3 kupitia msafara wa Malawi lakini pia kwa sasa, Taasisi inaendelea kufuatilia utekelezaji wa mikataba na makubaliano ya kibiashara iliyosainiwa katika matukio mbalimbali yaliyoratibiwa na TanTrade.”

Tantrade kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imejipanga kufanya mambo mbalimbali ikiwemo; kuendelea kuratibu shughuli za utafutaji masoko na ukuzaji biashara ili kuunganisha wazalishaji, kuendelea na taratibu za uanzishwaji wa Dawati la Waambata wa Kibiashara kwenye Ubalozi mbalimbali wa kimkakati wa Tanzania nje ya Nchi, kuendeleza ushirikiano na Ubalozi nje ya Nchi katika kutangaza fursa za masoko ya bidhaa na mazao yanayozalishwa nchini, kuratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2025 Osaka, Japani.

Previous articleRAIS. DKT. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MSHAURI WA MWANAMFALME WA SAUDI ARABIA
Next articleWADAU SEKTA YA UVUVI WAMSHUKURU DKT.SEMIA KULETA AGRF TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here