Home BUSINESS TASAC YAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI VYOMBO VYA MAJI

TASAC YAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI VYOMBO VYA MAJI

Na Mwandishi Wetu, Geita

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) halikubaki nyuma kutoka elimu kwa wachimbaji wa madini wa mkoa wa Geita na maeneo jirani kuhusiana na usafirishaji wa mashine, mitambo na vifaa vinavyotumika katika shughuli zao za kuchimba madini.

Mbali na hilo TASAC imewatoa hofu watumiaji wa usafiri maji na kuwahakikishia usafiri huo uko salama kwakuwa shirika hilo liko kazini masaa 24 yanapotokea majanga.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano Mwandamizi TASAC, Amina Miruko wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mkoni Geita katika maonesho ya madini.

Amesema moja ya majukumu ya shirika hilo ni kuhakikisha kuna udhibiti bora katika huduma zinazotolewa katika bandari pamoja na usafirishaji kwa njia ya maji, jukumu hilo wanalifanya kwa mujibu wa kifungu cha12 cha sheria ya uwakala wa meli sura ya 415.

Ameainisha katika utekelezaji wa majukumu hayo malengo makuu ni kudhibiti sheria hiyo ni kuchochea ushindani katika watoa huduma wanatoa huduma zenye tija na bora kwa wanaowahudumia.

Pili kulinda maslahi ya wateja pamoja na watoa huduma inatusaidia kutokuwa na migogoro na kutatuliwa na kupatiwa ufumbuzi kulinda maslahi ya watoa huduma, pia kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi vigezo na sheria za shirika.

“Katika kutekeleza jukumu hilo kuna maeneo mawili ambayo kwanza katika udhibiti wa huduma za bandari na usafiri kwa njia ya maji,  katika usafiri huo tunao mawakala wa forodha tunao wakala wa mali, wakusanyaji na watawanyaji wa mizigo,wahakiki shehena.

Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kalvin  akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati alipotembelea katika banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye maonesho ya Teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita, Katikati ni Afisa uhusiano Mwandamizi TASAC Amina Miruko na kushoto ni Victoria Myonga Afisa Udhibiti Huduma za Bandari TASAC.

 

Kwa mujibu Sheria ya uwakala  wa meli Tanzania sura 415 ilianza kutekelezwa Februari 23,2018 chini ya Wizara ya Uchukuzi walianza kutekelezwa majukumu pamoja na uhakikishaji wa kusimamia usalama wa vyombo vya abiria na mizigo ikiwemo mazingira. Amesema katika kaguzi Tasac ina kitengo chai kuratibu utafutaji na uokoaji.p

Amesema pia Tasac inafanya kazi ya biashara ya meli katika meneo 17 lakini kutokana na mabadiliko ya sheria ikapelekea na kupunguziwa sasa inafanya kazi katika maeneo matano tu ambayo ni makinikia,vipuri ama machine mbalimbali zinazotumika kufanya kazi ama uchimbaji katika maeneo ya migodi, mbili ni silaha na vilipuzi ikiwemo na wanyamapori.

Akianisha majukumu ya TASAC amesema waliwahi kutembelea katika miala ya visiwa mkoani Geita na maeneo mengine  kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya vifaa vya uokoaji wakati wa hatari. 

Naye Afisa Huduma za Bandari TASAC Victoria Miyonga amesema majukumu ya hudua za bandarinikiwemo na kutoa, kuhuisha na kufuta leseni za watoa huduma katika sektanya bandari na kwa usafiri njia ya maji.

Kuweka na kudhibiti vigezo na masharti ya utoaji huduma zinazodhibituwa na TASAC.

Kuweka kanuni na masharti ya kifuatwa na watoa huduma wanaodhibitiwa na Tasac.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi TASAC Martha Kelvin amesema maonyesho hayaua sita kwao yana toja kubwa kwani elimu kwanwachimbaji na wamiki wa vyombo majini wanatakiwanwapewe elimu stahiki kuhusiana nnshurika hili

“Lengo la ujio wetu nìkuhakikisha tunakuja kuwapa elimu wachimbaji na wamikiki kuhusiana na maukumu ya Tasac” amesema.

Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakiwa katika picha ya pamoja katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.

Previous articleATAKAYEKWAMISHA WAFANYABIASHARA NI ADUI NAMBA MOJA WA SERIKALI – Dkt. HASHIL
Next articleKATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here