Home BUSINESS TANZANIA INA FURSA NYINGI ZA UKWEZAJI SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI –...

TANZANIA INA FURSA NYINGI ZA UKWEZAJI SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI – ULEGA

Na: Grace Semfuko, MAELEZO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema Tanzania ina fursa nyingi za Uwekezaji kwenye Sekta ya uzalishaji wa chakula cha mifugo na kuwataka wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali Duniani kuja kuwekeza kwenye eneo hilo.

Ameyasema hayo wakati akifungua Mjadala kuhusu fursa za Uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi kwenye Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika- AGRIF linaloendelea Jijini Dar es Salaam.

“Tuna uwepo wa ardhi ya kutosha ya kilimo ambayo utaipata kupitia Taasisi zetu za Serikali kikiwepo Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC  ambayo inaweza kusaidia uzalishaji wa mbegu za malisho ya mifugo na soko linalopatikana kwa urahisi la mifugo na mazao ya mifugo nchini Tanzania yenye idadi ya watu milioni 61, soko la kikanda katika EAC na SADC na Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) lenye watu zaidi ya bilioni 1.4.”amesema

Mhe.Ulega Amesema pia Tanzania imeboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa baadhi ya kodi, ada na vikwazo visivyo vya ushuru katika biashara ya mifugo na mazao yake ambapo pia kuna mazingira mazuri na tulivu ya kisiasa na uwepo idadi kubwa ya rasilimali watu ikiwa ni pamoja na vijana na wanawake katika uzalishaji katika sekta ya mifugo.

Aidha amebainisha kuwa lengo la Tanzania ni kuweka mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji katika sekta ya mifugo ikihusisha ajenda ya fursa za ajira kupitia ushirikishwaji wa vijana na wanawake katika mwamvuli wa ‘kujenga kesho bora’ kupitia Wajasiriamali wa Mifugo na Uvuvi (BBT-LIFE).

Amezitaja faida za kuwekeza katika uzalishaji wa chakula cha mifugo ambapo amesema ripoti ya lishe ya kimataifa inaonyesha kuwa kuwekeza katika lishe ya mifugo ndio kichocheo cha gharama nafuu zaidi cha maendeleo na ustawi kwani kila dola moja inayowekezwa katika lishe inazalisha dola 16 kama malipo. Mwisho.

Previous articleYALIYOJIRI MAGAZETINI LEO SEPTEMBA 6-2023
Next articleTANZANIA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA MAONESHO YA 68 YA VITO THAILAND
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here