Home BUSINESS SERIKALI YATOA VIBALI KAPUNI 5 ZA WAZAWA KUCHIMBA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

SERIKALI YATOA VIBALI KAPUNI 5 ZA WAZAWA KUCHIMBA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya uchimbaji wa Makaa ya mawe mradi wa Mchuchuma iliyofanyika Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha ndoto ya utekelezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma inatimia na rasilimali hizo zinawanufaisha wananchi wote na kuchangia katika uchumi wa nchi.

Waziri Kijaji ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya uchimbaji wa makaa ya mawe mradi wa Mchuchuma iliyofanyika Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Shirika la Taifa la maendeleo (NDC) katika kutekeleza miradi ya Liganga na Mchuchuma na kwamba kuanza kwa uzalishaji kutaongeza ajira za moja kwa moja na za muda mfupi kwa wananchi.

“Mafanikio haya ni dhamira ya dhati na ya hali ya juu ya serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha ndoto za utekelezaji wa mradi wa liganga na Mchuchuma sasa zinatimia, na rasirimali hizi ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kuwanufaisha wananchi,  ziwanufaishe na kuchangia katika uchumi wa nchi” amesema Dkt. Kijaji.

Aidha, Dkt. Kijaji ametumia fursa hiyo kuwataka wawekezaji wazawa waliopewa leseni za uchimbaji wa makaa hayo, kutumia muda waliopewa kwaajili ya kufanya uchunguzi na hatimaye kuanza uzalishaji na kwamba kutofanya hivyo wananweza kupokonywa vibali.

Pia Dkt. Kijaji ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuchangia katika mafanikio hayo ambapo hapo awali aliridhia kutoa kiasi cha shilingi Bilioni 15.4 za Kitanzania ikiwa ni malipo ya fidia kwa wanufaika ambao watapisha utekelezaji wa mradi huu.

“Kwa nyakati tofauti mheshimiwa Ris Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisema ni wakati sasa umefika kwa rasilimali iliyopo katika miradi ya kimkakati ya Liganga na Mchuchuma kuanza uzalishaji, na kwamba ni shauku yake kuona mradi huu wa muda mrefu unatekelezwa” amesema Dkt. Kijaji. 

Awali akiongea alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mwendeshaji Shirika la Taifa la maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema kuwa mchakato huo ulihusisha jumla ya Kampuni 25 ambapo jumla ya ya Kampuni 17 ziliwasilisha maombi yao kwaajili ya uchambuzi na ushindani, ambapo kati yao Kampuni 5 zilikidhi vigezo.

“Kampuni ishirini na tano zilipewa nyaraka za zabuni zilipewa nyaraka za zabuni kupitia mfumo wa ununuzi Serikalini (TANePS), ambapo Kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za zabuni” amesema Dkt. shombe.

Pia, amebainisha kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kiuchumi ikiwemo kutoa ajira zaidi ya 500 za moja kwa moja, kurahisisha upatikanaji wa nishati inayotokana na makaa ya mawe kwa viwanda jambo litakalochochea ukuaji wa viwanda nchini pamoja na kuingiza fedha za kigeni kwa mkaa utakao uzwa nje ya nchi.

Jumla ya Kampuni tano zimetia saini makubaliano ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika mradi wa mchuchuma kwa miaka mitano. Kampuni hizo ni pamoja na Sheby Mix Investiment Limited, Nipo Engireering Company Limited, Chusa Mining Company Limited, Kindaini Company Limited, na Cleveland Mine Service Company Limited.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here