Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA ATEULIWA  MJUMBE WA BODI YA USHAURI YA KITUO CHA...

RAIS DKT. SAMIA ATEULIWA  MJUMBE WA BODI YA USHAURI YA KITUO CHA DUNIA CHA UHIMILIVU WA MABADILIKO YA TABIANCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteuliwa rasmi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Advisory Board of the Global Centre on Adaptation – GCA).

Taarifa ya uteuzi huo iliwasilishwa na Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa Bodi ya GCA na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na Mhe. Rais pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Nairobi, Kenya.

Heshima hii ni utambuzi wa uongozi mahiri wa Rais Samia katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Afrika na duniani kote ambapo Tanzania ni kinara kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali barani Afrika.

Previous articleMAJALIWA KUZINDUA RASMI MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUSAIDIA WAWEKEZAJI
Next articleSERIKALI YATOA VIBALI KAPUNI 5 ZA WAZAWA KUCHIMBA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here